Na Baraka Mbolembole
KIUNGO mshambulizi wa timu ya Taifa ya Zanzibar, Suleimani Kassim ‘Selembe’ amemaliza mkataba wake kama mchezaji wa Stand United lakini anajiandaa kukatisha mapumziko yake Zanzibar ili kwenda Shinyanga kutazama ofa ya mkataba mpya ambayo klabu hiyo imejiandaa kumpa.
“Mkataba wangu na Stand tayari umemalizika na wameniita niongeze ila kwa sasa nipo nyumbani Zanzibar kwa mapumziko. Nitaenda kuuangalia kama utakuwa na maslahi mazuri kwangu hakuna kipingamizi nitasaini,” anasema Selembe alipozungumza na mtandao huu mapema siku ya Alhamis hii.
Tayari Haruna Chanongo amesaini mkataba mpya wa miaka miwili katika timu hiyo inayotawaliwa na migogoro ya kimaslai.