SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumapili, 24 Julai 2016

T media news

Mwigizaji Jackline Wolper atangaza kuhama CHADEMA na kijiunga na CCM

Mwigizaji wa filamu nchini Tanzania Jackline Wolper aliyakuwa akimuunga mkono Edward Lowassa katika uchaguzi Mkuu 2015, ametangaza kujiunga na CCM rasmi jana

Wolper alikaribishwa na mwenyekiti aliyemaliza muda wake Dkt Jakaya Kikwete baada ya kutangaza kujiunga na CCM.

Kitendo hicho kilifanyika katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM uliofanyika jana Julai 23, mkoani Dodoma.

 

MSANII WALPER AMKIMBIA LOWASSA NA KUREJEA CCM


Msanii wa Bongo Movie, Jacqueline Walper usiku wa leo ameamua kurejea Chama cha Mapinduzi na kumkimbia aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa.


Walper ambaye alizunguka mikoani kumnadi Lowassa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 amewaomba radhi wafuasi wa CCM akidai aliteleza tu pale alipoamua kukipigia debe Chadema kipicha hicho cha uchaguzi.


Walper ametangaza rasmi uwamuzi huo kwenye Tamasha la Usiku wa Wasanii walipokuwa wakimuaga Jakaya Kikwete kwa kustaafu uenyekiti wa CCM.


PICHA ZOTE NA EDWIN MJWAHUZI