SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 23 Julai 2016

T media news

Home » Kitaifa » SAA CHACHE BAADA YA JPM KUWA MWENYEKITI CCM,ZITTO KABWE AMWANDIKIA WARAKA HUU..!!! SAA CHACHE BAADA YA JPM KUWA MWENYEKITI CCM,ZITTO KABWE AMWANDIKIA WARAKA HUU


Kiongozi wa chama cha ACT wazalendo, Zitto Kabwe amempongeza Rais John Magufuli kwa kuchanguliwa kuwa mwenyekiti wa CCM wa tano. 
Napenda kumpongeza Rais Magufuli kwa kuchanguliwa kwake kuwa kiongozi wa chama chake akiwa mwenyekiti wa CCM wa tano wa chama hicho. 
CCM imeendelea kudumisha utamaduni wa kukabidhiana uongozi kila baada ya muda, jambo ambalo ni la kujifunza hasa kwa vyama vya siasa nchini na barani Africa. Nataraji kwamba Rais na Mwenyekiti mpya wa CCM ataona umuhimu wa vyama vya siasa kuendelea kufanya siasa bila vikwazo na kwa mujibu wa sheria za nchi yetu. 
Demokrasia inaimarisha amani kwa kupaza sauti ya HAKI.. karibu kwenye changamoto za kuongoza vyama vya siasa ndugu Rais.