Mwanamuziki kutoka DRC, Koffi Olomide aachiwa huru siku moja mara baada ya kuhukumiwa kifungo cha miezi 18 jela mjini Kinshasa, kwa tuhuma za kumpiga teke dansa wake kike katika Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Jomo Kenyatta siku ya ijumaa, Julai 22.
Msanii huyo wa Lingala ameachiwa huru leo Julai 28 saa 4 asubuhi, na hii ikiwa ni shinikizo kutoka kwenye kampeni zilizofanywa na mashabiki wake mitandaoni kwamba ameonewa kwani alikuwa anawalinda wachezaji wake dhidi ya mwizi aliyekuwa karibu nao na lakini baadae akakiri na kuomba msamaha kwa makosa yake kwa mashabiki wake na wanawake wote duniani.
Alilala rumande usiku huo wa ijumaa alivyowasili nchini Kenya na kesho yake kurudishwa nyumbano kwake Congo na kukamatwa tena na polisi wa nchi hiyo mnamo Julai 25 na kupelekwa tena rumande mpaka siku hukumu yake ilipotoka ya kwenda jela miezi 18.
Aidha, Hii haikua mara ya kwanza kwa Mwanamuziki huyo kuhusishwa na vitendo vya vurugu kwenye mitandao. na livha ya hayo alichawahi kutuhumiwa kwa kosa la kumfanyia vurugu meneja wake na makosa matatu ya jaribio la ubakaji kwa madansa wake.