Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya mabadiliko madogo katika safu ya wakuu wa mikoa na amewateua wakuu wa wilaya 139.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika mabadiliko hayo Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Bi. Zainab R. Telack kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Bi. Zainab R. Telack anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Anna Kilango Malecela ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Rais Magufuli pia amemteua Dkt. Binilith Satano Mahenge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
Dkt. Binilith Satano Mahenge anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabit Mwambungu ambaye amehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es salaam ambako atapangiwa majukumu mengine.
Aidha, Rais Magufuli amemteua Dkt. Charles F. Mlingwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Dkt. Charles F. Mlingwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Stanslaus Magesa Mulongo ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Wakuu wapya wa mikoa walioteuliwa wataapishwa tarehe 29 Juni, 2016 saa tatu kamili asubuhi Ikulu Jijini Dar es salaam na mara baada ya kuapishwa watakula kiapo cha maadili ya uongozi.
Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya 139.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika uteuzi huo Rais Magufuli amezingatia mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na umri ambapo kwa wale ambao umri wao ni zaidi ya miaka 60 ameamua wastaafu.
Mhe. Rais amewashukuru sana kwa utumishi wao mzuri na amesema pale ambapo itahitajika, serikali itaendelea kuwatumia katika majukumu mengine.
Katika uteuzi huo, Wakuu wa Wilaya waliopo sasa ambao wamebaki katika nafasi zao ni 39. Pia Rais Magufuli amewateua Wakurugenzi Watendaji wa halmashauri 22 kuwa Wakuu wa Wilaya kutokana na utendaji wao mzuri.
Aidha, nafasi 78 za uteuzi wa Wakuu wa wilaya zimejazwa na watanzania wengine ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza wengi wao wakiwa ni vijana, wenye elimu ya kutosha na uzoefu katika maeneo mbalimbali
Walioteuliwa kuwa wakuu wa wilaya ni kama ifuatavyo (Orodha imepangwa kulingana na mikoa)
ARUSHA
Arusha - Mrisho Mashaka GamboArumeru - Alexander Pastory MnyetiNgorongoro - Rashid Mfaume TakaLongido - Daniel Geofrey ChongoloMonduli - Idd Hassan KimantaKaratu - Therezia Jonathan Mahongo
DAR ES SALAAM
Kinondoni - Ally HapiIlala - Sophia MjemaTemeke - Felix Jackson LyavivaKigamboni - Hashim Shaibu MgandilwaUbungo - Hamphrey Polepole
DODOMA
Chamwino - Vumilia Justine NyamogaDodoma - Christina Solomon MndemeChemba - Simon Ezekiel OdungaKondoa - Sezeria Veneranda MakuttaBahi - Elizabeth SimonMpwapwa - Jabir Mussa ShekimweliKongwa - John Ernest Palingo
GEITA
Bukombe - Josephat MagangaMbogwe - Matha John MkupasiNyang'wale - Hamim Buzohera GwiyamaGeita - Herman C. KipufiChato - Shaaban Athuman Ntarambe
IRINGA
Mufindi - Jamhuri David WilliamKilolo - Asia Juma AbdallahIringa - Richard Kasesela
KAGERA
Biharamulo - Saada Abraham MallundeKaragwe - Geofrey Muheluka AyoubMuleba - Richard Henry RuyangoKyerwa - Col. Shaban Ilangu LissuBukoba - Deodatus Lucas KinawiloNgara - Lt. Col. Michael M. MtenjeleMissenyi - Lt. Col Denis F. Mwila
KATAVI
Mlele - Rachiel Stephano KasandaMpanda - Lilian Charles MatingaTanganyika - Saleh Mbwana Mhando
KIGOMA
Kigoma - Samsoni Renard AngaKasulu - Col. Martin Elia MkisiKakonko - Col. Hosea Malonda NdagalaUvinza - Mwanamvua Hoza MlindokoBuhigwe - Col. Elisha Marco GagistiKibondo - Luis Peter Bura
KILIMANJARO
Siha - Onesmo BusweluMoshi - Kippi WariobaMwanga - Aaron Yeseya MmbagoRombo - Fatma Hassan ToufiqHai - Gelasius ByakanwaSame - Rosemary Senyamule Sitaki
LINDI
Nachingwea - Rukia Akhibu MuwangoRuangwa - Joseph Joseph MkirikitiLiwale - Sarah Vicent ChiwambaLindi - Shaibu Issa NdemangaKilwa - Christopher Emil Ngubiagai
MANYARA
Babati - Raymond H. MushiMbulu - Chelestion Simba M. MofunguHanang' - Sara Msafiri AllyKiteto - Tumaini Benson MagessaSimanjiro - Zephania Adriano Chaula
MARA
Rorya - Simon K. ChachaSerengeti - Emile Yotham NtakamulengaBunda - Lydia Simeon BupilipiliButiama - Anarose NyamubiTarime - Glodious Benard LuogaMusoma - Dkt. Vicent Anney Naano
MBEYA
Chunya - Rehema Manase MadusaKyela - Claudia Undalusyege KittaMbeya - William Ntinika PaulRungwe - Chalya Julius NyangiduMbarali - Reuben Ndiza Mfune
MOROGORO
Gairo - Siriel Shaid MchembeKilombero - James Mugendi IhunyoMvomero - Mohamed Mussa UtaliMorogoro - Regina Reginald ChonjoUlanga - Kassema Jacob JosephKilosa - Adam Idd MgoyiMalinyi - Majula Mateko Kasika
MTWARA
Newala - Aziza Ally MangosongoNanyumbu - Joakim WangaboMtwara - Dkt. Khatibu Malimi KazunguMasasi - Seleman Mzee SelemanTandahimba - Sebastian M. Walyuba
MWANZA
Ilemela - Dkt. Leonald Moses MassaleKwimba - Mhandisi Mtemi Msafiri SimeonSengerema - Emmanuel Enock KipoleNyamagana - Mary Tesha OnesmoMagu - Hadija Rashid NyemboUkerewe - Estomihn Fransis Chang'ahMisungwi - Juma Sweda
NJOMBE
Njombe - Ruth Blasio MsafiriLudewa - Andrea Axwesso TsereWanging'ombe - Ally Mohamed KassigeMakete - Veronica Kessy
PWANI
Bagamoyo - Alhaji Majid Hemed MwangaMkuranga - Filberto H. SangaRufiji - Juma Abdallah NjwayoMafia - Shaibu Ahamed NundumaKibaha - Asumpter Nsunju MshamaKisarawe - Happyness Seneda WilliamKibiti - Gulamu Hussein Shaban Kifu
RUKWA
Sumbawanga - Dkt. Khalfan Boniface HauleNkasi - Said Mohamed MtandaKalambo - Julieth Nkembanyi Binyura
RUVUMA
Namtumbo - Luckness Adrian AmlimaMbinga - Cosmas Nyano NshenyeNyasa - Isabera Octava ChilumbaTunduru - Juma HomelaSongea - Polet Kamando Mgema
SHINYANGA
Kishapu - Nyambonga Daudi TarabaKahama - Fadhili NkuluShinyanga - Josephine Rabby Matiro
SIMIYU
Busega - Tano Seif MweraMaswa - Sefu Abdallah ShekalagheBariadi - Festo Sheimu KiswagaMeatu - Joseph Elieza ChilonganiItilima - Benson Salehe Kilangi
SINGIDA
Mkalama - Jackson Jonas MasakoManyoni - Mwembe Idephonce GeofreySingida - Elias Choro John TarimoIkungi - Fikiri Avias SaidIramba - Emmanuel Jumanne Luhahula
SONGWE
Songwe - Samwel JeremiahIleje - Joseph Modest MkudeMbozi - Ally Masoud MaswanyaMomba - Juma Said Irando
TABORA
Nzega - Geofrey William NgudulaKaliua - Busalama Abel YejiIgunga - Mwaipopo John GabrielSikonge - Peres Boniphace MagiriTabora - Queen Mwashinga MloziUrambo - Angelina John KwingwaUyui - Gabriel Simon Mnyele
TANGA
Tanga - Thobias MwilapwaMuheza - Mhandisi Mwanaisha Rajab TumboMkinga - Yona Lucas MakiPangani - Zainab Abdallah IssaHandeni - Godwin Crydon GondweKorogwe - Robert GabrielKilindi - Sauda Salum MtondooLushoto - Januari Sigareti Lugangika
Wakuu wote wa Wilaya walioteuliwa wanapaswa kufika Ikulu Dar es salaam siku ya Jumatano tarehe 29 Juni, 2016 saa tatu kamili asubuhi kwa ajili ya kiapo cha maadili ya uongozi na maelekezo mengine kabla ya kuapishwa na wakuu wa mikoa watakaporejea katika mikoa yao.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
26 Juni, 2016