SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 6 Mei 2016

T media news

ANGALIA KIKOSI BORA ZAIDI CHA PAMBA YA MWANZA 'TP LINDANDA'



 Nakukumbusha, hii ndiyo Pamba ya Mwanza enzi hizo, timu yenye uwezo mkubwa na wachezaji ambao kama leo wangekuwa wanacheza, basi Ulaya ni kunusa tu.

Waliocheza Simba enzi hizo waulize kikosi hiki, TP Lindanda au Wana Kawekamo.

Waliosimama toka kushoto: Madatta Lubigisa, Rajabu Musoma, Beya Simba, Nteze John ‘Lungu’, Kitwana Selemani ‘Popat’, Fumo Felician, Pascal Mayala na Paul Rwechungura.

Waliokaa toka kushoto:George Gole, Khalfan Ngassa, Ally Bushiri, Alphonse Modest, Mao Mkamy ‘Ball Dancer’, Saleh Muhammad, Hamisi Nyembo na Nico Bambaga

Kilichofuata baada ya hapo: Madatta alistaafu akiwa Pamba, Beya na Nteze walitua Simba, Fumo na Mayala walienda Yanga, Gole alibaki Pamba, Ngassa na Ball Dancer walitua Simba, Modest alienda Simba kisha Mtibwa Sugar, Bambaga alienda Malindi kisha Simba.7