Kikwapa ni tatizo la kutoa harufu mbaya sehemu ya kwapani katika mwili wa binadamu. Tatizo la kikwapa husababishwa na bakteria wanaovutiwa na jasho au unyevunyevu chini ya kwapa.
Tatizo la Kikwapa ni kero kwa sababu husababisha mtu kutoa harufu inayokuwa kero kwako na kwa mtu mwingine aliyeko jirani yako.
Ili kwapa lako liwe na harufu nzuri, kavu na safi fanya yafuatayo;
1. Paka kipande cha limao kwenye kwapa na kuacha lipate hewa safi ili kuua vijidudu na kutoa tezi za jasho kuondoa harufu mbaya;
2. Vaa nguo safi zenye nyuzinyuzi za asili kama pamba, hariri na sufu zitasaidia kufyonza unyevu na kuliacha kwapa lako kavu, safi na bila harufu mbaya;
3. Oga kila siku na safisha nguo kwa maji safi itasaidia kuua bakteria na ambao husababisha harufu mbaya;
4. Kunywa maji mengi kila siku yatakusaidia kutoa sumu mwilini na hivyo kupunguza harufu mbaya ya kwapa;
5. Osha kwapa mara kwa mara kwa kutumia sabuni zenye dawa (medicated soaps);
6. Punguza kula chakula chenye viungo vingi hasa vitunguu;
7. Kumbuka kutumia pafyume na Spray zitasaidia kuondoa harufu mbaya kwa muda na sio kutibu tatizo moja kwa moja;
8. Baada ya kuoga jifute kwa taulo au kitambaa safi na usiache unyevu unyevu ambao uwavutia bakteria kukua katika eneo ili;
9. Jitahidi kunyoa nywele za sehemu hii mara kwa mara;
10. Epuka kukaa sehemu zenye joto kupita kiasi kwa muda mrefu.
Kama umenielewa SHARE na marafiki waelimike