Mahakama ya Tanzania imeingia Mkataba na Shirika la Posta Tanzania kutoa huduma za usafirishaji wa nakala za hukumu, barua na nyaraka muhimu za Mahakama.
Mkataba huo ulisainiwa na Mtendaji Mkuu wa Mahakama na Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta mapema Aprili 05 katika Ofisi ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama Mahakama ya Rufani-Dar es Salaam.
Mkataba huu chini ya huduma mpya ya Posta mlangoni (The post at your doorstep) iliyoanzishwa na Shirika la Posta hivi karibuni, utalipa jukumu la kukusanya na kusafirisha/kusambaza nakala za hukumu na nyaraka mbalimbali za Mahakama na kuzifikisha kwa wahusika kulingana na anwani zao na mahali walipo (Anwani za makazi).
Akizungumza kabla ya utiani saini wa mkataba huo, Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Bw. Hussein Kattanga amesema kuwa hatua hii ni mwendelezo wa maboresho mbalimbali yanayoendelea kufanyika ili kuwafikia wananchi.Aidha; Mtendaji Mkuu amelitaka Shirika hilo kutekeleza makubaliano hayo kwa ufanisi, ikiwa ni pamoja na kusambaza nakala za hukumu na nyaraka nbyingine kwa wahusika na kwa wakati.
“Sitarajii kuona wananchi wanapanga foleni Mahakamani kutafuta hukumu zao na nyaraka nyingine, nina imani kuwa Posta mtafanya kazi ya kukusanya na kusambaza nyaraka hizo kwa wananchi ipasavyo,” alisema Mtendaji Mkuu.Naye Msajili Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati ameeleza kufurahishwa kwake na utiaji saini wa Mkataba huo kwani utasaidia kufikia ndoto ya Mahakama ya muda mrefu ya kuwafikia wananchi kwa karibu zaidi.
“Naomba kusema kuwa, nimefurahishwa sana na hatua hii , kwani ni ndoto ya Mahakama ya muda mrefu, vilevile hatua hii itarahisisha utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Jaji Mkuu ya kutoa nakala za hukumu bure kwa zitawafikia wananchi popote watakapokuwa,” alisema Mhe. Revocati.Kwa upande wake Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Hassan Mwang’ombe alisema alimuhakikishia Mtendaji Mkuu wa Mahakama kuwa watafanya kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa.
“Kusainiwa kwa Mkataba huu kutawezesha pia kuongeza kasi ya usambazaji wa barua za kawaida za Mahakama kuwafikia walengwa mapema zaidi kwani zitachukuliwa Mahakamani na Maofisa wa Posta na kupelekwa moja kwa moja kwa wahusika/mhusika,” alisema Bw. Mwang’ombe.
Vilevile Mkuu huyo alitoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa Maofisa wa Posta hususani kwa kuandika anwani za makazi pamoja na postikodi.
Hafla hiyo fupi ilihudhuriwa na baadhi ya Maafisa Waandamizi kutoka Mahakama ya Tanzania pamoja na Shirika la Posta Tanzania.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang’ombe, akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba kati ya Posta na Mahakama ya Tanzania wa huduma ya Posta Mlangoni inayotolewa na shirika hilo. Hafla hiyo, imefanyika katika Ofisi za Mahakama ya Rufani, jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Katanga na kushoto ni Mwanasheria Mkuu wa TPC, Zuhura Pinde. Waliosimama nyuma yao, ni baadhi ya Maofisa waandamizi wa Posta na Mahakama.
Msajili wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati (kulia), akizungumza katika hafla hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang’ombe na katikati ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Katanga. Wengine nyuma kutoka kushoto ni Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara wa TPC, Fadya Zam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TPC, Elia Madulesi, Mtendaji wa Mahakama Kuu, Leonard Magacha, Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta na Mtendaji wa Mahakama ya Rufani, Solanus Nyimbi.
Msajili wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati (kulia), akizungumza katika hafla hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang’ombe na katikati ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Katanga. Wengine nyuma kutoka kushoto ni Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara wa TPC, Fadya Zam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TPC, Elia Madulesi, Mtendaji wa Mahakama Kuu, Leonard Magacha, Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta na Mtendaji wa Mahakama ya Rufani, Solanus Nyimbi.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Katanga akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mwanasheria wa Mahakama ya Tanzania, Peace Mpango (kulia), akisaini mkataba huo, huku akiangaliwa kwa makini na Mwanasheria Mkuu wa TPC, Zuhura Pinde.
Mwanasheria Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Zuhura Pinde, akisaini akisaini mkataba huo, huku akiangaliwa kwa makini na Mwanasheria wa Mahakama ya Tanzania, Peace Mpango.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang’ombe (kushoto) na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Katanga (kulia), wakibadilishana mkataba huo, mara baada ya kusainiwa katika hafla hiyo.