SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumapili, 8 Aprili 2018

T media news

KISA CHA KWELI


"Mke wangu alikua na mimba ya mwanaume mwingine na ndoa yangu ndiyo ilikua na siku saba tu, alitaka kunibambikizia lakini nikagundua. Baada ya kusoma ushauri wa wengi nilikaa muda mrefu kidogo bila kuchukua maamuzi yoyote, nilipanga nisimuambie mke wangu chochote na kuvumilia, lakini nilijua kitu kimoja, mke wangu alikua anaongea na Dada yake

EHivyo kama ningeliacha hilo suala yake akaongea basi watu wangejua na ningeaibika, nisingeweza kuvumilia kama ulimwengu ungejua nalea mtoto wa mtu mwingine. Niliamua kuongea naye na kumuambia nimejua mimba ile si yangu, mwanzo alibisha lakini baada ya umbana sana alikubali na kuanza kuomba msamaha. Mpaka naongea naye nilishakubali kumsamehe kwani sikuona kama naweza kumuacha wakati ndoa changa.

Nilimuambia aniambie ukweli wote na kama ataacha kitu basi nikija kujua sitamsamehe tena. Aliniambia kila kitu na nilimuamini, kubwa nikuwa aliniambia huyo mwanaume walikutana naye siku moja tu alitoka na marafiki na alilewa hakufikiria, nilimuambia kama huyo mwanaume anajua kama ana mimba yake alisema hapana, nilimuuliza mara kumi kumi akasema hapana, mtu pekee ambaye anajua kuwa ana mimba yake ni Dada yake tu.

Nilimuambia sawa, kama ni hivyo basi namuomba kitu kimoja. Aongee na Dada yake na kumuambia kuwa alipiga mahesabu vibaya na mimba ni ya kwangu, pamoja na kwamba ilikua inaniuma sana lakini kwangu ilikua ni bora kulinda uaneume wangu. Nilimuambia asimuambie chochote kuhusu mazungumzo yetu na hiyo ndiyo itakua siku ya mwisho kuyazungumzia na nilijua haitaleta shida kwani kila mtu alikua anajua ni wapenzi wa muda mrefu.

Alikubalia na hilo na nilimuacha aongee na Dada yake. Lakini kwakua sikua na muamini tena niliamua ku-hack simu yake, upande wa Whatsapp ili kuona meseji zake, nilitaka kuthibitisha kama kweli hawasiliani na huyo mwanaume. Nilichokiona ndiyo kimenifanya nije kwenu kuwapa mrejesho hapa, kwanza tu baada ya kuongea naye siku hiyo hiyo (ilikua usiku) alianza kuchat na Dada yake.

Binafsi nilimuambia amtafute waongee naye ila alianza kumtumia meseji, alimuambia nimejua kuwa mimba si yake, lakini nimemsamehe. Sasa badala ya kumuambia Dada yake kuwa alihesabu tarehe vibaya kama nilivyomuambia yeye alimuambia “Kanisamehe sema hataki mtu ajue, ameniambia hata wewe nikuambie nimehesabu tarehe zangu vibaya hivyo naomba chonde chonde usijemuambia mtu hili ufe nalo Shogaa!”.

Nadhani hapo mmeelewa alichokifanya, kwamba kwa Dada yake mtoto hawezi tena kuwa wangu. Niliendelea kufuatilia meseji zao, hakua akichat na huyo mwanaume lakini wakati wanachat Dada yake alimuuliza “Sasa na flani (akitaja jina la huyo mwanaume wake) utamuambiaje, si ulimuambia kuwa una mimba yake?” Yeye alimjibu “Anajua ila alinipa hela nikatoe, natafuta namna ya kuongea naye ili huyu asijue, kabla sijakata kabisa mawasiliano naye kuna hela alini promise, hope atanipa nianze hata kabiashara!”

Waliendelea kuchat sana (mambo mengine ambayo si muhimu hapa) lakini nilitaka muone uongo wake kwamba kumbe sio tu kwamba huyo jamaa yake anajua lakini pia bado wanawasiliana. Nilikaa kwa wiki moja nikitafakari nini cha kufanya, nilitamani kuwashirikisha watu na kuongea na ndugu zake lakini mwisho nilishindwa, niliamua kuwa mwanaume na sikuhitaji tena ushauri wa mtu mwingine.

Niliamua kumuonyesha zile meseji, aliishia kulia na kuniomba msamaha, lakini nilimuambia kama mwanzoni ambavyo nilikusamehe kabla ya kuniomba msamaha, mpaka nakuja kuongea na wewe nilishafanya maamuzi. Siwezi kukusamehe tena hivyo nataka tuachane, sitaki nikuumize na kukuharibia watu kukuona kuwa umeolwa na umeachika hapana, ninaweza kukupa muda wa kuendelea kukaa hapa mpaka ujifungue.

Kama ukitaka basi unaweza kukaa hapa na ukishajifungua basi utatafuta sababu yoyote ya mimi na wewe kuachana, utasingizia chochote utaondoka na tutaachana kwa amani kabisa, lakini suala la kuwa kama mke na mume hilo hapana, nitakua nakudanganya nikikuambia naweza kukusamehe tena. Aliomba msamaha sana lakini ananijua, nilishaamua na huo ndiyo uamuzi wangu wa mwisho.

Baada ya kumuambia hivyo niliendelea na mambo kama kawaida, Dada yake alinifuata kuongea na mimi lakini nilimuambia kuwa siwezi kuendelea kuishi naye na hilo jambo nishamalizana na mke wangu. Sijui walishauriana nini lakini jana nilipigiwa simu kalazwa Hospianini, kumbe aliamua kuitoa ile mimba na ikamletea shida, mimba kashatoa lakini siamini kama naweza kumsamehe kwani sikutaka kumuacha kwasababu ya mimba bali kwasababu ya usaliti na uongo.

Nimeenda kumsalimia na namuaombea Mungu atoke (leo anaweza kutoka) na naamini pia leo ndiyo itakua mwisho wa ndoa yetu kwani nilikua tayari kumpa mwaka mwingine ili ajifungue kabla ya kuondoka lakini kwakua kashaamua kuwahi kujifungua naamini nitakua nimefanya jambo sahihi kuendelea na maisha yangu. Nimeamua kuwashirikisha kwani bado najiuliza je nitakua nimemuonea, je niko sawa kuachana naye, anahitaji nafasi nyingine kweli?"
#babad said

Nategemea ushauri wenu kwa namba 0784699901