SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 7 Aprili 2018

T media news

KATIKA SWALA LA BANGI MSIPOTOSHE KAULI YA MH RAIS



Na Thadei Ole Mushi.

#Watu wanataka kutafsiri Kauli ya Rais vibaya kuwa si haki wanakijiji wakafyeke shamba la Bangi kwa kuwa sio wao wameotesha. Kuna mambo matatu ya msingi mbayo kama umeumbiwa kupinga utapinga tu lakini yana manufaa makubwa sana.

1.#Wanapotosha kwa makusudi alichomaanisha Rais ni kuwa haiwezekani Shamba liwe kijijini kwenu, kuna mwenyekiti wa kijiji, kuna Mtendaji wa Kijiji na viongozi wengine halafu Mtu aanzishe shamba alime, aoteshe na avune halafu shamba hilo linakuwa halijulikani ni la nani. Wanakijiji kuambiwa kuwa watafyeka ni sahihi kabisa na wanatakiwa kupata adhabu zaidi ya kufyeka ikiwezekana hata watendaji na nwenyekiti mpaka mjumbe wa nyumba kumi wafungwe tu.

2. #Maana ya pili ni kuwa Jeshi la polisi linatakiwa liongeze weledi kuliko kufyeka kila siku wawatambue watu hao wanaolima. Rais kawakumbusha kazi yao ya msingi ya intelligence ambayo kazi hiyo ikifanyika kwa umakini tutatokomeza swala hilo kabisa. Kazi ya polisi si kusafisha makosa ya wahalifu bali kazi yao ya kwanza ni kukamata wahalifu.

3. #Tatu Rais amejaribu kutuma ujumbe kwa wanaofanya kazi kwa kutafuta Kick. Ndio maana kashangaa mpaka baadhi ya MaRPC Kuonekana na slesha wakifyeka. Raisi anatoa ujumbe kuwa kinachotakiwa ni weledi na watendaji  watambue job description.

#Msiwe watu wa kupinga tu kila kitu muwe mnaangalia kwa mapana jambo kabla ya kuongea.

Ole Mushi