Ili kunogesha mahusino ya kimapenzi lipo japi kubwa sana ambalo unatakiwa kulifahamu na jambo hilo si jingine bali ni kuhakikisha unakuwa ni mtu mwenye kuomba msamaha hasa pale unapokesea.
Wanaume wengi wanaamini kwamba hata wakikosea, hawatakiwi kuomba msamaha kwa sababu kuomba msamaha ni ishara ya udhaifu, matokeo yake wanaendekeza mfumo dume bila kujua kwamba mapenzi ni demokrasia!. Ambapo kila pande ni lazima mmoja wapo ajue kanuni na misingi ya kujishusha hapa pale anapokosea.
Bila kujali kwamba wewe ni mwanaume au mwanamke, mkubwa au mdogo, una fedha au huna, inapotokea umeziumiza hisia za mwenzi wako, iwe kwa jambo dogo au kubwa, ni lazima uombe msamaha na kuahidi kutorudia makosa.
Ukishajenga utaratibu huu, hata kama mwenzi wako hakuwa na kawaida ya kuomba msamaha, taratibu utambadilisha. Utashangaa na yeye anaomba msamaha na huo unakuwa mfumo wa maisha yenu. Kuwa makini kwamba ukiomba msamaha leo, siyo kesho unarudia tena kosa lilelile, ataona unamfanyia makusudi.
Ukizingatia jambo hilo ukazidisha mapenzi na kumjali mwenzi wako, ukawa mwaminifu na mkweli, hisia tamu za mapenzi unazozihisi leo, ni lazima utafutrahia mahusiano yenu.