SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 14 Machi 2018

T media news

Haji Manara afunguka kuachana na Klabu yake

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Klabu ya Simba SC, Haji Manara amefunguka na kusema kwa sasa ameamua kuachana na klabu yake ya Manchester United hadi Kocha wa klabu hiyo Jose Mourinho atakapoondoka.

Haji Manara amesema hayo siku moja baada ya klabu yake hiyo kupigwa bao 2 kwa moja na klabu ya Sevilla hivyo Manchester United kuondolewa kwenye mashindano ya klabu bingwa ulaya.

"Guys kuna vitu siwezi kuviasi..1.Dini yangu,,2.wazazi wangu..Mke na watoto wangu na Simba...ila Manchester nimeiacha hadi Mourinho aondoke...Europe nimebaki na Madrid tu.....Kwangu Jose ndio mtu wa hovyo kupita wote duniani kwa sasa" alisema Haji Manara

Siku tatu zilizopita wakati Manchester United ikikipiga na Liverpool aliahidi kama timu yake itafungwa angehama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuhamia CHAUMA lakini baahati nzuri timu yake ikashinda ila baada ya kupigwa na Sevilla ameamua kukaa pembeni mpaka kocha Jose Mourinho atakapoondoka.