SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 15 Februari 2018

T media news

Shilole Arudi Kwao Igunga..... Atoa Msaada Katika Shule Aliyowahi Kusoma

Moja kati ya jambo la msingi ambalo wasanii na watu maarufu wamekuwa wakilifanya ni kurudisha fadhila kwa jamii ambapo wengi wao wamekuwa wakitoa misaada katika shule au vituo vya watoto wanaoishi maisha magumu, Shilole ameingia kwenye list ya mastaa walioamua kurudisha fadhila kwa jamii..

Shilole ametoa msaada wa Pen, Penseli pamoja na vifutio kwa wanafunzi wa shule ya Igunga aliyosoma kuanzia darasa la kwanza mpaka la saba ambapo baada ya kutoa zawadi hizo alipost kwenye ukurasa wake wa instagram na kuandika.

…>>>“Mapema jana nilikuwa shule ya msingi Igunga ambayo nilisoma hapo kuanzia la kwanza mpaka la saba! Kukumbuka ulipotoka ni jambo jema sana na kuchangia kidogo niliwapa zawad ya pen! Pensel! na vifutio asante Flaviana Matata foundation kwa kunisaport kwa hili 🙏🙏” – Shilole