Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa amefunguka na kuweka wazi kuwa endapo Waziri wa Maliasili na Utalii atatoa ushahidi wowote ambao unaonyesha yeye ana masilahi na makampuni ya uwindaji atajiuzulu nafasi yake ya ubunge.
Mchungaji Msigwa amesema hayo Februari 12, 2018 kupitia moja ya mitandao yake ya kijamii na kudai kuwa Waziri huyo amekuwa ni muongo na ni mtu ambaye hajiamini
"Kigwangalah ni muongo anyependa masifa, ni mtu asiyejiamini. Kama akitoa ushahidi wowote utakaodhihirisha kuwa nina masilahi na makampuni ya uwindaji nitajiuzulu ubunge .Nina wasiwasi na upbringing yake" aliandika Msigwa
Mbunge Msigwa amesema hayo kufuatia kauli ambayo Waziri Kigwangalla aliitoa siku chache zilizopita kupitia mtandao wake wa Twitter kuwa Mbunge huyo wa Iringa Mjini anahusika na ana hisa katika vitalu, jambo ambalo Msigwa mwenyewe amelipinga vikali na kuamua kuweka ubunge wake rehani endapo Waziri huyo atathibitisha hilo.