SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumapili, 11 Februari 2018

T media news

Mwaka 1985, Thomas Sankara alikaririwa akisema kuhusu falsafa yake kisiasa



 Na MWINYI,HALID

Mwaka 1985, Thomas Sankara alikaririwa akisema kuhusu falsafa yake kisiasa kwamba:

‘you cannot carry out fundamental change without a certain amount of madness’, yaani hauwezi kuleta mageuzi ya msingi bila kuwa na kiasi fulani cha ukichaa... Ndipo mabeberu na Vibaraka wakaeneza propaganda kwamba Sankara ni KICHAA anayeingoza Burkina Faso.....Wapinzani ndani na nje ya nchi wakasikika "Sankara anaua Demokrasia"

Sankara akasema "ukitaka kujua maana ya ubeberu angalia sahani yako ya chakula, utaona kila aina ya chakula unachokula kinatoka nje. Ndipo akahimiza Afrika ijitegemee kwa chakula, akisema: "Anayekulisha anakutawala"

Kama ilivyokuwa kwa Robert Mugabe wa Zimbabwe,Thomas Sankara akachukua Ardhi iliyokuwa imeporwa na Mabeberu na kuigawa kwa wakulima wadogo huku akisisitiza kwamba hata yale madeni ya Afrika hayana uhalali kwa vile yalitokana na mikataba mibovu na Ndio maana hakuna maendeleo yaliyotokana na mikopo ya kigeni na kuitaka Afrika iache kulipa madeni yasiyolipika....ni wakati huo huo Mwalimu Nyerere naye alikuwa amesema kwamba Mtu hawezi kulipa madeni wakati watoto wanakufa njaa.

Kwa hatua hizo ni wazi Sankara aliwakasirisha sana mabeberu wa kimagharibi, hasa ubeberu wa Kifaransa uliokuwa ukitawala kupitia vibaraka wake wa Afrika kama Rais Felix Houphouet- Boigny wa Ivory Coast....Sankara akawa amewaudhi wakubwa wa dunia (mabeberu) kwa kukataa kwake mipango ya kurekebisha uchumi ya Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha Duniani (IMF) huku hoja kubwa ya sankara ikiwa ni kwamba, mipango hiyo ni ya kinyonyaji.

ikumbukwe Sankara alikataa hata picha yake (yeye kama Rais) kutundikwa katika majengo, na taasisi za serikali.. alisema hataki kutukuzwa, na katika kuhakikisha kuwa rasilimali za nchi zinahudumia wanachi wa kawaida alipambana na rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma, huku akimtaka kila mwananchi kuchapa Kazi na kujituma kulijenga taifa...alichukia rushwa na ufisadi, uvivu, uzembe, dhuluma na unyonyaji wa wananchi na rasilimali zao. Alitaka kuona watu wake wakifaidika kwa rasilimali za nchi yake.

Ndani ya Burkina Faso Haya ni baadhi ya Mambo aliyoyafanya Thomas Sankara aliyejulikana kama Che – Guevara wa Afrika..

Alianzisha kampeni ya kuboresha Elimu na kutanua
Huduma za Afya kwa watu wa Burkina Faso maeneo ya vijijini hasa kwa watoto walio athirika na magonjwa ya Uti wa mgongo , Homa ya manjano, na surua.. na watoto karibu milioni 3 walipata tiba hizo.. Alianzisha kampeni ya upandaji wa miti kitaifa, na takribani miti Milioni kumi ilipandwa nchi nzima..

Pia alianzisha kampeni ya usafi nchini kote, kila mwananchi alipaswa kufanya usafi eneo alipo.. na Sankara mwenyewe alikuwa anashika fagio na kuingia barabarani kufanya usafi.. Hiyo ni kampeni iliyoitwa mfagio wa mwananchi (le balai citoyen).

Aliongeza idadi ya wanawake katika serikali yake, ikiwa ni kampeni yake nchi nzima kupinga tohara kwa wanawake na kusisitiza Usawa wa Kijinsia huku ndoa za wasichana wadogo na za kulazimishwa haswa za kimila katika maeneo mengi ya Burkina Fasso zikapigwa marufuku..

Akiwa kama Rais wa nchi, alivaa nguo zilizotengenezwa Burkina Faso badala ya suti kutoka Paris na London.. mara nyingi alionekana akiwa kwenye gwanda la jeshi.

Alifuta matumizi ya magari ya kifahari kwa viongozi na watumishi wote wa umma, yeye kama Rais alikuwa akitumia baiskeli au miguu kwenda kwa wananchi vijijini kuhimiza na kusimamia shughuli za kimaendeleo..

Alijikita sana kwenye kusimamia na kukuza sekta ya afya katika Burkinabe, alihimiza watu kujihusisha na kilimo.. akiwapelekea zana za kilimo na pembejeo bure kwa watu wa vijijini na kugawa ardhi kwa wananchi ili wajihusishe na kilimo..

Kwa muda mfupi sana akiwa kama Rais wa Burikna Fasso, aliweza kuifanya nchi hiyo kuagiza chakula kutoka nchi za nje na kuifanya nchi hiyo kuanza kuuza vyakula vyake nje.. akaanza kuifanya Burkina Fasso kuwa imara kiuchumi huku akiwahimiza watawala wa Afrika waache kuwaibia wananchi, waache kutegemea sadaka kutoka nje.

Huyu ndiye Thomas Sankara ambaye alipunguza mshahara wake hadi dola 450 kwa mwezi (Laki tisa na Ushee) na kumfanya kuwa Rais anayepokea Mishahara Mdogo zaidi Afrika huku akitembelea baskeli katika mitaa bila ya kulindwa. Alipoulizwa kwanini hana walinzi alisema wananchi ndio walinzi wake, hivyo hahitaji kuambatana na wanajeshi wenye bunduki...( hili ndilo Kosa kubwa alilofanya, akawa anawindwa bila kujua) na hata aliposhauriwa atumie Gari kwa Usalama wake achagua Renault  badala ya Msururu wa Mashangingi ..

Hata hivyo Sankara bado alibaki na baiskeli yake mpaka alipokutwa na mauti, huku akaunti yake ya benki ikikutwa na akiba ya dola 400 ambayo ni sawa na Tsh 850, 550/= (laki nane elfu hamsini na tano namia tano hamsini),

Thomas Sankara alidumu kwenye uongozi wake kwa kipindi cha miaka 4 pekee kabla ya mapinduzi yaliyoongozwa na Rafiki yake kipenzi... Blaise Compaore akishirikiana na Mabeberu wa Kifaransa..Mapinduzi ambayo yaliondoka na uhai wake kwa kuvamiwa na kupigwa Risasi Nyingi mwilini akiwa Ikulu akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri...Ndoto ya Burkina faso ikafa.

Ndoto kubwa ya kila siku ya Thomas Sankara, ilikuwa ni kuifanya Burkina fasso kuwa moja kati ya mataifa makubwa Afrika kiuchumi...Nchi ambayo aliibadili jina kutoka jina la wakoloni "Upper Volta" kuwa "Burkina Faso" akimaanisha "Ardhi ya Watu wenye Akili"...huku akipokea mshahara wa dola 450 kwa mwezi, mshahara mdogo kuliko viongozi wote barani Afrika kwa wakati huo...." MUNGU ibariki Afrika"


Je leo viongozi wa afrika hii ,tupo wapi?```