Matokeo ya awali ya uchaguzi wa ubunge Jimbo la Kinondoni yaliyobandikwa nje ya vituo vya kupigia kura yanaonyesha mgombea wa CCM, Maulid Mtulia anazidi kuongoza katika baadhi ya vituo.
Katika matokeo hayo, Mtulia anafuatiwa na mgombea wa Chadema, Salum Mwalimu huku wa CUF, Salum Rajab Juma akishika nafasi ya tatu lakini kwa tofauti kubwa ya kura.
Baadhi ya matokeo hayo ni kama ifuatavyo; Kituo cha Mbuyuni 3 Kata ya Tandale, Mtulia amepata kura 53, Juma 3 na Mwalimu 18.
Kituo cha Mashuka 2 Kata ya Tandale, Mwalimu amepata kura 16, Juma 7 na Mtulia 53.
Kituo cha Mashuka 1 Kata ya Tandale, Mtulia amepata kura 59, Mwalimu 14 na Juma 3.
Kituo cha Ofisi ya Mpakani -7 Kata ya Ndugumbi, Mtulia amepata kura 33, Mwalimu 20, Juma 6 na mgombea wa Tadea 1.
Kituo cha Mpakani -3 Kata ya Ndugumbi, Mtulia amepata kura 49, Mwalimu 14, Juma 16 na mgombea wa Tadea 1.
Kituo cha Serikali ya Mtaa Bwawani 4 Kata ya Kijitomyama, Mtulia amepata kura 237, Mwalimu 21 na Juma 1.
Kituo cha Bwawani 01 Kata ya Kijitonyama, Mwalimu amepata kura 23 na Mtulia 100.
Kituo cha Bwawani 2 Kata ya Kijitonyama, Mtulia amepata kura 37, Mwalimu 24 na Juma 1.
Kituo cha Weo 1 Kata ya Makumbusho, Mtulia amepata kura 35, Mwalimu 20 na Juma 3.
Kata ya Sokoni Makumbusho A-1 Kata ya Kijitonyama, Mtulia amepata kura 30, Mwalimu 12 na Ashiri Saidi 1.
==Matokeo zaidi yanaendelea kutangazwa