SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 10 Februari 2018

T media news

HOTUBA YA MWENYEKITI UVCCM TAIFA KWA BARAZA LA UVCCM MKOA WA MWANZA


"Fanyeni kazi kwa mujibu wa Kanuni, mliomba kuwa tumikia vijana, watumikieni kwa nguvu zote".
# M/Kiti UVCCM Taifa.


"Siasa za Mwanza nazifahamu, fanyeni siasa za Nguvu na za kisayansi"
#M/Kiti UVCCM Taifa.

"Leo mnachagua wajumbe wa kamati ya utekelezaji Mkoa, chagueni wajumbe wabunifu wenye maono na wenye kulinda Mali za Jumuiya Mkoa wa Mwanza".
# M/Kiti wa UVCCM Taifa.

"Baada ya uchaguzi wa leo wa kamati ya utekelezaji Mkoa wa  Mwanza, Wajumbe mtakao wa chagua wanahaki ya kupata Bank statement, wajue Jumuiya inanini, Wanahaki ya kujua Mali za Jumuiya ziko wapi? na Zinasaidiaje Vijana?
# M/Kiti UVCCM Taifa.

"Naomba Mchague Wajumbe wenye weledi, wachapa kazi watakao mshauri Mwenyekiti wetu wa Mkoa vizuri, Msiogope kuivunja  kamati ya utekelezaji kama itashindwa kutimiza malengo mliyo jipangia, Hakika UVCCM  Mkoa wa Mwanza naifahamu.
#M/Kiti UVCCM Taifa.

" Shirikianeni Vizuri, Semeaneni Vizuri kwa maana ushirikiano wenu utawafanya muwe mashujaa, hakika hamjui kesho Nani atakuwa Nani na wapi.
#M/Kiti UVCCM Taifa.

 "Baraza la Vijana Mkoa wa Mwanza lililomaliza muda wake lilitoa Viongozi thabiti kwa serikali yetu, Je? Baraza hili limejipangaje? Ni lazima mchape kazi, Hakika Walioteuliwa na Mh. Rais kutoka kwenye Baraza la Vijana Mkoa wa Mwanza walichaguliwa kwa sababu ya Weledi na Uchapa kazi wao.

# M/Kiti UVCCM Taifa.

 "Jifunzeni kumaliza matatizo yenu ninyi Vijana, ni marufuku matatizo yenu kujadiliwa na Viongozi wa serikali, kwani Makatibu wa CCM wa Mikoa huwa hamuwaoni?
#M/Kiti UVCCM Taifa.

 *"Shirikianeni, Saidianeni, Pendaneni hamuwezi kujua nani atakuwa wapi kwa msaada wa nani..*

#M/Kiti UVCCM Taifa.

"M/Kiti wa UVCCM Mkoa wa Mwanza ni Jonathani Lufungulo, Mkome kuandika barua Makao makuu juu ya kuomba uchaguzi urudiwe.. Huyu mwenyekiti wenu wa Mbao wa kuchonga asubiri 2022.

# M/Kiti UVCCM Taifa.


"Nguvu mnazotumia kumalizana leo, ndio hizo hizo zitakazo tumika kumalizwa nyie kesho.

#M/Kiti UVCCM Taifa
[2/10, 14:16] Maandazi: Hakikisheni mnaipitia mikataba yote ya Mali za Jumuiya Mkoa wa Mwanza.

# M/Kiti UVCCM Taifa

"Nataka kuiona Jumuiya ya UVCCM Mkoa wa Mwanza ikisonga mbele na sivinginevyo.

# M/ Kiti UVCCM Taifa

 "Hakikisheni mnaibua miradi mipya kwa mustakabali wa UVCCM Mkoa wa Mwanza.. Ni lazima muwe wabunifu.
# M/Kiti UVCCM Taifa