SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 21 Februari 2018

T media news

Diamond aanza kusaka watangazaji wa Wasafi TV na Radio

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva anayehit hapa nchini, na sehemu mbalimbali nje ya nchi, Diamond Platinumz hatimaye ameanza kusaka watu wenye vipaji vya utangazaji wa reddio na runinga ili waanze kufanya kazi katikamkituo cha runinga na redio cha Wasafi.

Msanii huyo, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram ameandika “Please tell me, From your perspective which City has the best Radio and Tv Presenters…? Eti nna swali…Hivi ni Mkoa Upi Una Vipaji sana vya Watangazaji?”

 

Hivi karibuni Diamond alitangaza kuanzisha kituo cha runinga na redio cha Wasafi TV na Wasafi Radio ambacho kitakuwa katika jengo la makao makuu ya WCB lililopo Mbezi.

Diamond aliwahi kueleza kuwa kupitia kuanzishwa kwa redio na Tv hiyo ya Wasafi, ataweza kutoa ajira kwa vijana mbalimbali.

Hata hivyo bado hajaweka wazi ni lini hasa kituo hicho kitaanza rasmi kurusha matangazo japo amewahi kuonyesha baadhi ya mitambo iliyoko ndani ya kituo hicho ikiwa imekamilika.