BUNGE la Afrika Kusini limemchagua Mwenyekiti wa chama tawala cha ANC Cyril Ramaphosa, kuwa Rais wa mpito wa nchi hiyo, mpaka pale uchaguzi utakapofanyika baada ya rais wa taifa hilo Jacob Zuma kujiuzulu.
Zuma alikuwa akikabiliwa na tuhuma nyingi, moja ikiwa ni kumhusisha na vitendo vya rushwa japokuwa mwenyewe amekanusha kuhusishwa na tuhuma hizo.
Alijiuzulu mara moja jana jioni licha ya kusema hakubaliani na uamuzi wa chama.