TAARIFA YA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA UMEME MIKOA YA KANDA YA ZIWA
Tunawataarifu Wateja wetu wa Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Tabora na Mara kuwa kutakuwa na matengenezo katika njia kubwa ya umeme ya msongo wa kilovolti 220 na 133 siku ya Jumamosi Januari 27, 2018 kuanzia Saa 2:00 Asubuhi - 12:00 Jioni.
Kutokana na maboresho hayo baadhi ya maeneo ya Mikoa hiyo yatakosa umeme.
LENGO: Ni kuboresha hali ya upatikanaji umeme katika Mikoa hiyo.
Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.
Tafadhali usishike waya uliokatika toa taarifa kupitia simu zifuatazo:
Kwa mawasiliano
Kituo cha miito ya simu Makao Makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100
Tovuti: www.tanesco.co.tz, mitandao ya kijamii:
Mitandao ya kijamii
Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,
Facebook https://www.facebook.com/tanescoyetultd/
IMETOLEWA NA: OFISI YA UHUSIANO
TANESCO MAKAO MAKUU
JANUARI 24, 2018