Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemhukumu Salum Njwete maarufu kama ‘Scorpion’, kifungo cha miaka saba jela pamoja na faini ya shilimgi milioni 30, kwa makosa mawili ya kujeruhi pamoja na wizi.
Scorpion amesomewa hukumu hiyo leo Jumatatu, Januari 22, katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, baada ya kukutwa na hatia ya kumjeruhi Said Mrisho na kumsababishia upofu.
Mahakama hiyo imemtoza faini ya shilingi milioni 30, ambazo ametakiwa kuzilipa hapo hapoa, fedga ambazo atalipwa Said Mrisho, kama fidia kutokana na kujeruhiwa kwake.
Said Mrisho aliyepata ulemavu wa macho baada yakujeruhiwa na Salum Njwete ‘Scorpion’.
