SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 25 Januari 2018

T media news

Chuchu Hans Afunguka Sababu ya Kumtoboa Mtoto Wake Sikio

MUIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Chuchu Hans amefungukia madai ya kumtoboa sikio mtoto wao wa kiume Jaden mwenye umri wa mwaka mmoja akidai kuwa suala hilo limepokelewa ndivyo sivyo.

Akizungumza na gazeti hili, Chuchu alisema kuwa hakumtoboa kabisa sikio bali baba yake (muigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’) ndiye aliyemvalisha kihereni cha kubandika na siyo kumtoboa moja kwa moja.

“Watu hawajatuelewa jamani hatuwezi kumtoboa sikio mtoto kwenye umri alionao tena wa kiume bali baba yake alimvalisha hereni ya kubandika tu, wasituzungumzie vibaya bwana,” alisema Chuchu.