Saudi Arabia Jumamosi imetangaza kuwakamata bilionea na muwekezaji maarufu Mwanamfalme Awaleed bin Talal pamoja na wanawafalme wengine wasiopungua 10 mawaziri wanne na makumi ya mawaziri wastaafu kwa tuhuma za rushwa
Kukamatwa kwa Mwanamfalme Alwaleed kumetikisa Saudi Arabia pamoja na vituo vya uwekezaji duniani
Anamiliki kampuni za za uwekezaji nchini humo na ni mmoja wa watu matajiri zaidi duniani akiwa anamiliki au ameshawahi kumiliki hisa nyingi katika mashirika ya habari, Citigroup, Twitter pamoja na makampuni mengine makubwa. Mwanamfalme huyo pia anamiliki mtandao wa televisheni unaotazamwa kwa eneo kubwa la Uarabuni
Kampeni hiyo ya kukamatakamata inaonekana kama njia ya kujiimarishia mamlaka ya mfalme mtarajiwa Mohammed bin Salman, mtoto wa Mfalme Salman
Akiwa na umri wa miaka 32 tu tayari mtoto huyo ana sauti kubwa kwenye jeshi la Saudi sera za kiuchumi, kijamii na za nje jambo linaloleta malalamiko katika familia ya kifalme kuwa amaejilimbikizia nguvu kubwa akiwa katika umri mdogo
Vituo vya ndege binafsi vilifungwa kwa ajili ya kuzuia wanawafalme wengine wasitoroke kabla ya kukamatwa