NAVY Kenzo kruu ya watoto wa kishua katika Afrika Mashariki, inaundwa Emmanuel Mkono ‘Nahreel’ na Aika Mareale. Mbali na kufanya Bongo Fleva katika level za juu, pia wanamiliki lebo ya The Industry iliyowahi kuwasainisha wanamuziki kadhaa wakiwemo Rosa Ree na Wildad.
Baada ya mwaka jana kutikisa na Albamu ya AIM (Above In A Minute) wakiwa na ngoma kadhaa ikiwemo Kamatia Chini, mwaka huu wameonekana kupunguza makeke. K
utokana na ukimya huo, Over Ze Weekend ilimsaka mmoja wa memba, Aika ambaye juzikati zilisambaa habari kuwa ni mjamzito ili aweze kufungukia sababu za ukimya wao, lakini pia ishu ya ujauzito, tetesi za kufulia na kuondokewa na wanamuziki wote ndani ya lebo.
Huyu hapa; Over Ze Weekend: Hongera kwa ujauzito Aika.
Aika: Asante, ni kweli kimeelewekaaa…hahahaa…
Over Ze Weekend: Unatarajia kujifungua lini?
Aika: Desemba 2, mwaka huu. Over Ze Weekend: Waoh! Mungu awe upande wako na bila shaka, mmekwishachungulia na kujua jinsi ya mtoto?
Aika: Ndiyo, ni mtoto wa kiume na jina lake ataitwa Gold.
Over Ze Weekend: Je, inawezekana suala lako la ujauzito ndilo limefanya Navy Kenzo kupotea kwenye gemu?
Aika: Siyo kweli. Hatujapotea, tupo tu kimya na tuliamua kuwa hivyo kutokana na hali yangu ya ujauzito.
Over Ze Weekend: Lakini hamuoni kukaa kimya kunawafanya kuwa mbali na ‘fansi’ wenu? Kwa nini usingekuwa kimya wewe mwenye ujauzito na Nahreel akafanya kazi kama kawaida.
Aika: Tunafanya kazi kama kundi na tumekuwa kimya labda kwa kutoa tu wimbo, lakini mbali na mimi kuwa kwenye hali hii, tunafanya shoo nyingi tu.
Over Ze Weekend: Unakwenda kuwa mama, je, nini
Over Ze Weekend: Je, kuna kitu special ambacho unaweza kuwaeleza mashabiki wenu, utajifungulia wapi na mmeandaa nini baada ya mtoto kuzaliwa?
Aika: Haaa… haaa,
surprise ni surprise tu. Watu wasubiri vitu vizuri havihitaji haraka.
Over Ze Weekend: Ni siri gani mnayo kwa kudumu kama kundi ilhali ni wapenzi?
Aika: Kuheshimiana, tunapokuwa kazini, mimi ninasimama kama Aika na Nahreel anasimama kama Nahreel na ndiyo maana tunaenda.
Over Ze Weekend: Mngependa mtoto wenu aje kurithi kipaji chenu?
Aika: Unajua hatuwezi kumchagulia ila akiwa mkubwa atachagua mwenyewe
kitabadilika kwenye kazi yako ya muziki? Aika: Hakuna kitakachobadilika. Aika ni yuleyule, suala la kuwa mama ni baraka nyingine kwenye maisha yangu.
Over Ze Weekend: Navutiwa kuendelea kuuliza, je, ni kweli kuwa ndiyo sababu pia ya wanamuziki wa lebo yenu kuwakimbia?
Aika: Si kweli, baadhi ya wanamuziki wetu tumewaondoa na wengine wameondoka wenyewe.
Over Ze Weekend: Kwa nini mmewaondoa?
Aika: Sitapenda kuzungumzia sana maana hilo limekwishapita.
Over Ze Weekend: Je, mmewaondoa au wameondoka wote?
Aika: Ndiyo! Navy
Kenzo ni Aika na Nahreel tu kwa sasa.
Over Ze Weekend: Vipi kuhusu kufulia? Je, ni kweli mmeshindwa kuendeleza ujenzi wa mjengo wenu wa ghorofa mliouanza kwa mbwembwe nyingi, kumudu kuendesha lebo na kuwahudumia wanamuziki walioondoka? Aika: Hili nalo ninalisikia kwako kwa mara ya kwanza.
Sisi hatujafulia, tunaendelea na biashara zetu na mambo yetu yanakwenda vizuri tu. Nikuambie tu kwa mwaka huu, Navy Kenzo wamefanya vitu vikubwa kuliko miaka mingine