UBUYU wa leo ni wa moto na hauna bei kwani upo kwenye punguzo maalum kutokana na hali ya sasa kifedha kuwa siyo shwari! Muuza nyago aliyeinogesha video ya mwanamuziki Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, Zena Abdalah ‘Jike Shupa’ yamemkuta. Ubuyu mtamumtamu wa mjini unamung’unywa kwamba, wiki iliyopita Jike Shupa alitolewa vyombo vyake nje kwenye nyumba aliyopanga maeneo ya Mwanyamala, Kwa-Manjunju jijini Dar, kisa kikidaiwa kuwa ni picha chafu anazotupia kwenye mitandao ya kijamii. Msambaza ubuyu huo alilitonya Ijumaa Wikienda kuwa, nyumba aliyopanga Jike Shupa inamilikiwa na watu walioshika Dini ya Kiislam.
KISA PICHA ZA UTUPU
Ilidaiwa kuwa, Jike Shupa ana tabia ya kutupia picha na video za utupu mitandaoni, jambo ambalo watu anaokaa nao hawalipendi na hata wapangaji wenzake hawataki mtu anayekwenda kinyume na maadili.
Habari zinazidi kudai kuwa, juzkati Jike Shupa alitupia video kwenye ukurasa wake wa Mtandao Kijamii wa Instagram, ikionesha wanawake wakicheza wakiwa utupu, jambo ambalo liliwakera mno watoto wa mwenye nyumba anayoishi. “Yaani ile nyumba anayoishi Jike Shupa ni ya watu walioshika dini sana, hawapendi kuona mtu anakiuka maadili, hata wapangaji waliowapangisha,” alisema mpashaji wetu huyo.
KUMBE ALISHAONYWA Mtoa Ubuyu huyo alizidi kubainisha kuwa, baada ya watoto hao kuona picha hizo walikereka kwa sababu mara kadhaa walishamuonya Jike Shupa kuwa hawapendi kupangisha mtu mwenye tabia kama hizo hivyo walipandwa na hasira na kumuomba aondoke, akatafute sehemu nyingine Chanzo hicho kilizidi kutiririka kuwa, baada ya watoto wa mwenye nyumba hiyo kutoa amri hiyo, Jike Shupa alianzisha timbwili akiwavimbia hivyo kuzidi kuwapandisha hasira na kuanza kurusha vitu vyake nje usiku wa manane. “Jike Shupa alikuwa akibishana nao huku wakirushiana maneno makali, jambo ambalo liliwakera watoto wa mwenye nyumba na kuamua kumtolea vyombo nje,” kilizidi kumwaga ubuyu chanzo hicho.
HUYU HAPA JIKE SHUPA
Baada ya gazeti hili kupata Ubuyu huo lilifanya jitihada za kumtafuta Jike Shupa ambaye alilielekeza Ijumaa Wikienda limfuate kwa rafiki yake. Alipoulizwa kuhusu ishu yake hiyo alikiri na kusema kuwa, mtu anapopanga nyumba na kumlipa mwenye nyumba fedha zake za pango, hapaswi kufuatiliwafuatiliwa. “Yaani wale watu walinizingua sana, mtu nimepangisha na fedha nimetoa, nini shida, nisitangaze shoo yangu? Sasa mimi nitakula wapi? Au fedha ya kodi nitapata wapi? Wala hawajaniumiza kabisa na nimeshapata nyumba nyingine,” alisema Jike Shupa.
NENO LA MHARIRI Jike Shupa ni staa hivyo anapaswa kuwa kioo cha jamii hivyo tukio lililomkuta linapaswa kuwa findisho kwa mwingine yeyote.