Takriban watu 50 wameuwawa katika shambulio la kujitolea muhanga katika maeneo ya Kaskazini Mashariki mwa mji wa Mubi.
Wakuu katika eneo hilo wanasema kwamba watu zaidi ya kumi wamejeruhiwa, baada ya mtu aliyejitolea muhanga kujilipua ndani ya msikiti mmoja wakati wa sala ya alfajiri Jumanne.
Mubi ni mji ulioko katika Jimbo la Adamawa, mahali ambapo wanamgambo wa Boko Haram, wamekuwa wakitekeleza mashambulio ya mara kwa mara.
Shahidi Abubakr Sule aliambia AFP kwamba inaonekana kwamba mlipuaji huyo alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakitekeleza ibada hiyo.
Hakuna mtu aliyetangaza kuhusika na ulipuaji huo lakini kundi la wanamgambo wa Boko Haram limekuwa likilenga makundi ya watu kaskazini mwa Nigeria.
Takriban watu 20,000 wameuawa katia kipindi cha miaka minane ya mashambulizi ya Boko haram.
Mwandishi wa BBC Ishaq Khalid ameripoti kwamba wanamgambo wa Boko Haram wameimarisha mashambulio yao katika eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria baada ya jeshi kuyakomboa maeneo yaliokuwa yakidhibitiwa na kundi hilo.
Takriban watu 45 waliuawa katika shambulio la bomu la kujitolea muhanga katika jimbo hilo hilo mwezi Disemba.
Katika shambulio hilo wanawake wawii wa kujitolea muhanga walijilipua katika soko ambalo lilikuwa limejaa watu.