Mkuu wa Mkoa na Jiji la Dar es Salaam anastahili pongezi kubwa za dhati kabisa kwa mkakati wake wa kuijenga Dar es Salaam mpya ambapo amekuwa akifanya kazi mbalimbali kubwa ambazo angetakiwa kuzifanya Waziri au Mbuge kwa mfano ktk suala la ujenzi wa viwanda, suala la vita ya madawa ya kulevya, ukarabati magari ya majeshi yetu, kuleta madaktari bingwa kutoka nchi za nje na kafanya ziara mara kadhaa jijini humo akisikiliza kero za wananchi na kuzitolea majibu papo hapo kwa kutumia wataalamu wake.
Hapa ndipo utaweza kugundua wasaidizi wa Rais Magufuli wababaishaji na wanaoendana na falsafa ya Ilani ya CCM ktk dira ya maendeleo ya Tanzania ya mwaka 2025. #Hapakazitu.
Kwa mjibu wa Dira ya Taifa letu kupitia chama tawala CCM kuelekea 2025, kati ya malengo makuu matano ya kitaifa yaliyotajwa, Makonda amekuwa mwangalifu ktk kuyatimiza kwa vitendo na kwa kiwango cha juu zaidi. Hakuna ambapo hajapagusa ktk utendaji na utekelezaji wake.
Tumezoea kuona wanasiasa wanaowawakilisha wananchi ktk vyombo mbalimbali, ikiwemo bunge na halmashauri ndio wanafanya vikao hivi kwa lengo la kupokea na kupeleka kero hizo kunakohusika.
Katika hali ya kawaida, mwanasiasa hatoi utatuzi wa kero hizo mwenyewe.
Lakini mkakati wa Makonda umetengeneza njia ya mkato ya kushughulikia kero za wananchi.
Makonda kama kiongozi wa serikali kwa msaada wa wataalamu wake anaweza kutoa majibu ya kero papo hapo.
Kinachofurahisha zaidi ni kuona kuwa Makonda amekuwa mkweli.
Tofauti na wanasiasa ambao panapotakiwa jibu kuwa 'hapana' atasema 'tutaangalia..' na hivyo kuwapa imani ya uongo wananchi, lakini Makonda amekuwa haogopi kusema hapana.
Sifa mojawapo ya kiongozi ni uwezo wa kusema "HAPANA".
Ukimwangalia Makonda, unatamani wakuu wote wa Mikoa na Wilaya wangekuwa na 'spirit' na mikakati ya ubunifu wa kazi kama yake, nafikiri hakuna Machinga, Mama ntilie na mwenye kioksi ambaye angesumbuliwa kodi na TRA wala migambo wa halmshauri, na taasisi nyinginezo kama osha, taka, bima, n.k wa mjibu wa mpango na kiwango cha kodi kuhusu nani anastahili kulipa na nani anastahili kusamehewa kodi.
Hii isingekuwapo kwa sababu viongozi wangebaini mapungufu ktk mahitaji ya maendeleo kiuchumi wa watu wao na kutumia plan "B", tulisema wadowadogo hawataguswa kwa mambo ya kodi kutokana na kipato chao kuwa chini.
Sasa imekuwa tofauti, kama mama ntilie amekopa pesa kwa sacos akakodi kibanda na bado kupitia mtaji huo alishe na kusomesha familia(watoto) wakati huo anatakiwa kulipa kodi zaidi ya nne ikiwemo TRA sidhani kama serikali inamuondolea umasikini huyo mtu maana kumwondoleaumasiki huyo ni pamoja na kumwezesha ajikwamue kiuchumi aweze kusomesha na kuishi kwa raha ktk nchi yake.
Makonda anashawishi wawekezaji ambao wanalipa kodi na kuajiri vijana ambao mwisho wa siku wanapata mitaji inayowawezesha kulipa kodi TRA, lakini sio hii inayowabana wajasiliamali wadogo kama sehemu ya kuendesha halmashari.
Sielewi na sina hakika sana viongozi wengine labda wanafanya vizuri huko waliko ila hayatangazwi maana wakuu wa Mikoa na Wilaya wa mijini wanakuwa na faida ya kuwa karibu na vyombo vya habari.
Umaarufu wa Makonda ni wa faida kijamii na wala jamii ya kitanzania isiwasikilize viongozi wabezaji kwa kuwa wao wamekosa ubunifu zaidi ya kuvizia maono au agizo la Rais.
Wapo wanaosema Makonda anapoteza muda na badala yake angefaa tu kufuatilia utekelezaji wa Ilani iliyowapatia kura, hizi ni hisia za kisiasa za wanasiasa wavivu wa kufikiri, maana licha ya uwepo wa Ilani, ni wajibu wa wawakilishi wa watu (wabunge na madiwani) kukutana na wananchi kuwasikiliza kero zao na kuwasemea na kuzitatua pia.
Pili, haihitaji akili nyingi kujua kuwa changamoto za wananchi zinabadilika.
Yaliyokuwa yakiwakwaza jana sio yale yanayowakwaza leo au yanaongezeka au yanapungua.
Kwa hiyo haki za msingi za wananchi haziwezi kuisha kamwe maana changamoto za maendeleo ni siku zote ni endelevu, ukiwapa leo haki wananchi wako kesho huwezi kuwakataza wasidai haki nyingine kwakua jana uliwapa zile, wataziomba tu kwa sababu leo zimeongezeka na ni haki zao za msingi.
Huwezi kuwanyima watu haki zao, haki hazina ukomo wa kuzidai hata kama zingemiminika kama mvua na hakuna mahali popote ktk katiba ya nchi yetu inasema au kutaja mwisho wa haki za msingi.
Kwa nini Makonda na kwa nini Mrisho Gambo?.
Kama kuna jambo naweza kushauri basi ningeshauri watendaji na viongozi wetu badala ya kuwaona Makonda na Gambo kitofauti lakini fundisho wanalolitoa si la utendaji wao bora pekee! bali ifahamike kuwa wao wako makini zaidi kuutambua mifumo, ukisikiliza malalamiko ya wananchi yanayotolewa mbele ya viongozi hawa utagundua kuwa kunaudhaifu ktk mifumo yetu ya utoaji haki na huduma mbalimbali ktk jamii.
Ninamaana kwamba, kujitokeza kwa watu wengi wenye malalamiko binafsi, wanaoshitaki ktk mikutano kudhurumiwa mali zao kama viwanja, nyumba, na vijikondi ambavyo havistahili n.k inaonyesha kuwa mifumo yetu bado si rafiki vya kutosha kiasi vya kuwawezesha wanyonge kufikisha malalamiko yao na kushughulikiwa hadi kupatikana suluhisho la hai.
Mifumo hii imelenga kuwanyonya na kuwagandamiza wananchi wanyonge kama ambavyo ilivyokuwa kwa tawala za kinyonyaji huko ulaya na marekani miaka ya ile ya kale.
Mifumo ya tawala hizo hazikuwaruhusu waumini wa kidini kuzifahamu sheria na miongozo za Biblia, kwa hiyo viongozi wa kidini walijipa mamlaka ya kusamehe na kufuta dhambi kwa watenda dhambi, na kuwadanganya kuwapa baraka, hivyo waumini walilazimika kutoa fedha nyingi ili kufutiwa dhambi zao na kupata eti 'baraka?'.
Mtakumbuka yaliyompata Martin Luther baada ya kuwapinga hao mataperi na wanyonyaji na mafisadi kwa kuwaambia kuwa hawana mamlaka ya kufuta dhambi za watu wenye dhambi bali ni Mwenyezi Mungu pekee.
Ujinga wa waumini wale ulitengenezwa na viongozi wa kidini ili wapate sehemu ya kufanyia ufisadi wao bila waumini kuujua ukweli.
Lakini ujinga wa watanzania wengi umetengenezwa na mafisadi tunayoyaamini ktk serikali zetu, wanafanya hivyo ili wananchi wasijue sheria za nchi wala haki zao za kiraia na za msingi.
Watanzania wengi hawana elimu ya kutosha juu ya sheria na namna ya kufikisha malalamiko yao kwa maana hawajui pa kwenda wala kujuzijua haki nyingine ambazo ni zao, kutokana na kutojua chochote kuhusu mambo mbalimbali na haya niliyoyataja watanzania wamegeuzwa kuwa mitaji ya mafisadi kwa makosa yao mbalimbali ya kijinga.
Makonda na Gambo na wengine wachache kwa mjibu wa Rais Magufuli wamekuwa kama Martin Luther kwa sababu wanachukiwa na wapiga dili kwa kufichua maovu ya watendaji mbalimbali mafsadi na wasiopenda kuwajibika kwa wananchi.
Kama viongozi wengi wangekuwa na dhamira njema na kwa dhati kulikuwa na haja shule zetu kuanzia msingi mpaka juu zingeweka kipaumbele ktk suala la watanzania kuzijua sheria badala ya kufanya hivyo kwa njia ya semina ya siku moja tu, mbaya zaidi sheria zenyewe zimeandikwa kwa lugha ya kigeni (kiingereza).
Hii inatofauti gani na waliopiga marufuku waumini wao kusoma biblia?, yaani sheria za waswahili ziandikwe kwa lugha isiyo yao ( kiingereza)? au wanasubili akina Martin Lutha wajitokeze ktk taifa hili?.
Jambo la pili ambalo ningeshauri, naona ipo haja ya elimu hii halmashauri zetu kuwa na vipindi vya redio, TV, Makala, gazeti, Mitandao na kuifikia jamii yenyewe moja kwa moja kuielimisha juu ya haki zao na kuwaelimisha sheria mbalimbali.
Ziara za akina Makonda na Gambo zimesaidia kuwamlikia watanzania mambo ya mifumo mibovu inayotunzunguka ktk jamii.
Tumeona namna wenyeviti wa vitongoji na wa vijiji na wa Mitaa walivyochukuliwa hatua na wengine kuswekwa ndani kwa sababu ya kutotumia risiti halali.
Wanapiga dili tu.
Nafikiri mpaka hapo utakuwa umenielewa msomaji maana yangu na dhana niliyotumia ktk makala haya.
Mwaandishi wa makala ni Kwiyeya Singu.