SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 21 Novemba 2017

T media news

KIFO SOMA HADI MWISHO TAFADHALI



Nikiwa katikati ya furahaa nikifurahia maisha kwani nilikua na kila sababu ya kufurahi ghafla hali isiyoweza kuelezeka ilinitokea
Nikashindwa kuwaita wapenzi na rafiki zangu ili wanisaidie ktk hali hiyo
Nikiwa katika mshtuko mkubwa na kufadhaika kwani sikutaraji kujijuta katika hali hiyo kwa kua nilikua mzima wa afya na mwenye furaha tele.  Hatimae imekua na huzuni na 😭😭😭😭 machozi kwa kua kila nilichokiwaza kiligeuka kua ni ndoto.  Tayari malaika wa mauti amesimama mbele yangu akanifungulia na kunionyesha mema yangu na pia mabaya yangu kwa hakika nilijiona kama vile nipo usingizini lakini kila kitu kilionyeshwa kwa uwazi na kwa uhakika
Nikiwa katika hali hiyo ya uchungu na maumivu ya kutolewa roho niliwaona ndugu na wapenzi wakiwa karibu yangu nilitamani walau kwa mapenzi yao kwangu ajitokeze mmoja wao kuchukua nafas yangu ili mimi niendelee kubaki na kupumua lakini kama vile hawakujua nini kimenipata kwani hata wao waligubikwa na majonzi na machzi yakiwatoka hawajui vipi wanisaidie
Kwahakika nilikua nikitamani walau nipewe muda kidogo ili nikaswali kwa unyenyekevu nikitamani nipewe muda kidogo tu nikatoe sadaka na pia nilitamani muda kidogo niweze kuisoma qur aan lakini yote hayo yalikua yako nje kabisa ya uwezo wangu
Nitolewa roho yangu ikachukuliwa huku nikiiangalia kwa macho yangu.  Mara sauti za ndugu na wapenzi wangu zilisikika ndani ya masikio yangu wakiulizana vipi tayari ameshakufa wakiwa katika hali ambayo hawaamini walianza kulia na kunifunga macho yangu 😭😭😭😭😭😭
Wakaagizia kitanda cha kamba na kukiweka karibu yangu kisha wakanibeba na kuniondoa juu ya kitanda changu wakanilaza juu ya kitanda cha kamba
Wakaagizia maji na kisha wakanivua nguo zangu
Nilitamani kuwazuia wasifanye hivyo nikiona aibu ya kufanyiwa kile ambacho nilipokua hai nilikifanya kwa kujificha na kujifungia mlango bafuni lakini katu sikuweza kumzuia hata yule alienitoa nguo yangu ya ndani na kisha kuanza kunimiminia maji huku wakiwa wamenifunika na shuka wakaniosha kama nilivyokua nikioga katika ile hali ya kujitwaharisha
Baada ya hapo ikaagizwa nguo yangu ya mwisho 😭😭😭😭😭😭 nguo ambayo sikupata kuijaribu kua inanitosha ama laa.  Nguo ambayo sikuwahi kupeleka kitambara kwa fundi ili nishonewe
Ni nguo kila mmoja hakubali kuivaa ktk uhai wake nayo ni sanda ambayo nilikafiniwa mwili mzima mwisho nikifungwa mfano wa pipi
Nikaingizwa ndani ya mkeka na kusokotwa.
Nikabebwa na kutolewa ndani ya nyumba yangu nikiwasikia wapenzi wangu wakinililia na kuniombea nilitamani walau niweze kuwakumbatia na kuwaaga kwa kua naelekea kwenye safari ya mwishoooo 😭😭😭😭😭😭
Safari ambayo nisingeweza kurejea tena.  Lakini sikuweza kuinuka tena nikatolewa na kupelekwa sehemu ambayo niliswaliwa swala ya ajabu kabisaa
Swala isiyokua na rukuu wala sujudu nikaombewa dua hapo kisha nikachukuliwa na kupelekwa maskani yangu ya milele hadi qiyaamah!!
niliingizwa katika qabr ambayo walau nitatamani kugeuka sikuti nafas ndani yake. Kutokana wembamba wa sehemu hiyo.  Bila ya kusita wale waliokua ni watu wa karibu zaidi ndio walikua wakwanza kuniwekea ubaoooo na hatimae kunimiminia tani za mchangaa.......Mchanga ambao lau niko hai natiliwa kwenye gunia niubebe nisingeweza kuubeba. Sikua na nguvu ya kuwazuia waliendelea kunimiminia mchanga walipomaliza waliondoka kwa unyongee wakirejea nyumbani wakiniacha sehemu ile ambayo sikua na hata rafiki wa kuongea nae nilijikuta kila kitu ndio kimefikia mwisho
Malengo yangu yaliishia njianii
Ndugu na rafiki zangu siwezi kuonana nao tena
Nilibakia kusubiri amri ya mola nini kitaendelea baada ya hapooo............

#TurudiniKwaMola
#TuelekezanePeponi....
#AllahAtupeMwishoMwemaNaAwarehemWaliotangulia..... AllahumaAmeen 😭😭😭😭