SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 19 Septemba 2017

T media news

Viwanda Zaidi ya 900 Htarini Kufutiwa Hati ya Mliki

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama amesema wameanza utaratibu wa kufuta hati miliki ya ardhi katika viwanja zaidi ya 900 ambavyo wamiliki wake wameshindwa kuviendeleza kwa zaidi ya miezi 36.

Mshama amesema jana Jumatatu kuwa ameshawasilisha barua kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ya kusudio la kuanza mchakato wa kufuta miliki katika viwanja 189 kwa ajili ya viwanda na taasisi mbalimbali.

Pia, miliki katika viwanja 754 vya watu binafsi baada ya wamiliki kushindwa kutekeleza maagizo waliyopewa ya kuviendeleza na wengine anuani zao hazijulikani.

Amesema hayo alipozungumzia utekelezaji wa agizo alilotoa mwezi uliopita kwa wawekezaji na watu binafsi kutumia siku 30 kuendeleza maeneo yao na kama kuna tatizo wafike kujieleza ili kupata muafaka.

Mkuu wa wilaya amesema waliotekeleza agizo hilo ni wamiliki wachache.

Wilaya ya Kibaha ambayo ni makao makuu ya Mkoa wa Pwani inakabiliwa na changamoto ya wawekezaji, taasisi  na watu binafsi kuhodhi maeneo na kutoyaendeleza hivyo kusababisha kuwepo mapori.