SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 15 Septemba 2017

T media news

USITAKE NDOA KWA PUPA MWISHO UKALIA NA TALAKAđź’”USIA WA MAMA KWA MABINT*

```Mwanangu nisikufiche, watu wengi huchangia sherehe ili waje kula na kunywa na kuoneshana fahari, ukoo wa Mume na ukoo wa mke nao wanaoneshana umwamba hawa kwenye Send-off na hawa wanajibu kwenye harusi.

Na ule usiku baada ya reception sijui ndio mnaita hivyo mnaingia kwenye gari kuelekea kwenye fungate.

Hapo hata wanakamati huwa wanakimbiana ninyi mkishaondoka kwani shughuli yao imeishia pale.

Hata wasimamizi watawasindikiza mpaka chumba mnacholala kisha wanawaacha hapo.

Lakini kazi yako ndio inaanzia hapo. Wewe humalizii siku ya harusi.

Hapa ndio unaosha make up na kubandua hizo kope
artificial na kucha na kuingia kwenye mapambano kupigania Ndoa yako.

Ukweli ni kwamba wanaotarajia NDOA itakushinda ni wengi nikiwemo Mimi mama yako jambo siombi hilo litokee , na tunapokupigia simu kuuliza "Mnaendeleaje? " huwa tunatarajia jibu lolote kutoka kwako.

Kwa sababu NDOA Inaanza baada ya harusi.

Usiingie huko ndani kwenda kucheza.

Naomba nikwambie kauli ngumu na ndio ukweli kwa sababu nakupenda Mwanangu .

Hicho cheti ni karatasi tu yenye nembo ya Taifa ili kukutambulisha kisheria kama mke wa Mtu.

Shetani hakiogopi wala wanawake wa nje hawakiogopi.

Na hizo Pete ni kama urembo vidoleni mwako, usidhani kuwa zimemfunga mume wako kufanya maamuzi magumu ikiwa utamvuruga kichwa.

Ukweli ni kwamba sijaona mwanaume anayeogopa cheti, labda wapo ila Mimi sijaona.

Nakushauri binti yangu usikose adabu ukajivunia Pete na cheti.

Hata kama mtajenga nyumba kwa majina yenu, mwanaume anapokosa amani anaweza kuacha ghorofa akaenda kupanga chumba kimoja uswahilini.

Usidhani wote wanaopaki magari huko kigogo na tandale huku wameacha nyumba zao bahari beach, zenye Jacuzzi na wanaenda kuoga kwa ndoo na kopo uswahilini, sio wote wamefungwa na uchawi.

Wapo wengi wamekimbia makelele na ugomvi usiokoma.

Mdomo wako unapaswa kuleta faraja kwa Mumeo na sio maumivu ya kupasua moyo wake.

Sheria ya maisha ni kuvuna unachopanda na asilimia kubwa ya wanaume hawasemi wanapoumia kupitiliza. Ila huingia kwenye mapango ya mioyo yao na kutunga sheria, akitoka huko hata uje na jeshi la malaika wa mbinguni na baragumu hutarudisha nyuma maamuzi atakayofanya.

Usijibweteke. Nyumba inajengwa na Mwanamke mwenye akili au kubomolewa na Mwanamke Mpumbavu. Yote yako mikononi mwako.

Ukitaka kupendwa pendeka, ukitaka kukalia kaa la moto, jifanye pasua kichwa.

Asili ya mwanaume ni games, ukianza kushindana naye na wewe unataka kibesi ligi haitaisha. Ila ukishuka na kukaa nafasi yako utadekezwa kama yai.

Namalizia na hili binti yangu

usimnange Mumeo, amekuamini mpaka kukufanya mkewe.

Anashambuliwa na kila kitu kwenye maisha yake.

Hebu msaidie nyumba yake iwe sehemu ya makimbilio.

Usimfanye moyo kupasuka kila anapowaza kurudi nyumbani utajitengenezea tabu ambazo kuzituliza itakuwia vigumu.

Hii NDOA ni yenu, usitumie mfumo wa mashost zako kuendeshea nyumba yako, wanaume hawafanani.

Ushauri mwingine uishie kwenye magroup usilete nyumbani.

Nimekwambia kitu,  ili NDOA yako ikadumu. Zaidi sana katika adhabu zote unazoweza kumpa Mumeo usimnyime tendo la Ndoa.

Huo mwili ni mali yake. Hizo moods zako ziishie sebuleni, kule chumbani wasilisha rejesho la siku.

Mwanangu  Hayo ukiyazingatia duniani hutoona adha ya ndoa.