SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 15 Septemba 2017

T media news

Rais Kenyatta aanza kufuata sera za Rais Magufuli

Ikulu ya Jamhuri ya Kenya imepiga marufuku kwa wafanyakazi/watumishi wote wa serikali kusafiri nje ya nchi bila ya kuwa na kibali maalumu kutoka kwa Rais.

Katika barua iliyotolewa Septemba 13 mwaka huu na Ikulu ya Kenya, ilieleza kuwa kuanzia sasa hadi itakapoamuliwa vinginevyo, hakuna mtumishi wa serikali atakayeruhusiwa kutoka nje ya nchi pasi na idhini ya Rais,

Kuondoa utata, barua hiyo iliwataka wahusika waliozuiwa kuwa ni, Makatibu Wakuu wa Baraza, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Makatibu Wakuu, Maafisa katika wizara, Wakurugenzi wa Mashirika na maafisa wengine, Bodi za Wakurugenzi wa Mashirika.

Katika barua hiyo, haikuelezwa sababu za serikali ya Kenya kuweka marufuku hiyo kwa viongozi wake.

Zuio kama hilo la Kenya, limewahi kuwekwa nchini Tanzania ambapo Rais Dkt Magufuli mara tu baada ya kuingia madarakani Novemba 5, 2015 alipiga marufuku safari zote za nje, na kwamba anayetaka kusafiri alihitajika kibali cha rais.

Rais Magufuli aliyeingia madarakani na mpango wa kupunguza matumizi ya serikali alisema baadhi ya viongozi wamekuwa hawafanyi kazi badala yake wanasafiri kila mara, jambo ambalo hawezi kulivumilia chini ya utawala wake.