SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 16 Septemba 2017

T media news

Mrundi anukia kurithi mikoba ya Phiri Mbeya City

Na Thomas Ngi’tu

Zikiwa zimepita siku chache Mbeya City itangaze kuachana na aliyekuwa kocha wao Kinnah Phiri, klabu hiyo tayari imeshaanza mchakato wa kutafuta mrithi wa mikoba ya kocha huyo.

Mbeya City hivi sasa inanolewa na Kijuso ambaye alikuwa kocha msaidizi msimu uliopita lakini tangu kuanza kwa ligi amekaimu nafasi hiyo baada ya Phiri kuchelewa kujiunga na kikosi hiko.

Taarifa zilizoifikia ShafihDauda.co.tz ni kuwa, tayari majina matano yameshafika mezani kwa uongozi wa klabu hiyo likiwemo jina la Ramadhan Nswazurimo raia wa Burundi ambaye anaitaka nafasi hiyo.

Makocha wengine ambao ShafifDauda.co.tz imezidaka juu kwa juu kuwa wapo katika mchujo wa majina matano ni Ally Bushiri, Muhibu Kanu, Maka Mwalwisi na Jabir aliyekuwa Kocha msaidizi enzi za Mwambusi.

Hata hivyo Mbeya City ambayo imetangaza kuvunja mkataba na kocha wao Kinnah Phiri, bado inapigana kuhakikisha wanamalizana katika suala la pesa za mkataba na kocha huyo.