SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 8 Septemba 2017

T media news

Fid Q Achafukwa na Wadada Wanaotegeshea Wanaume Mimba...Adai ni Ukatili na Dhuluma

Rapa Farid Kubanda 'Fid Q' ameibuka na kuwachana baadhi ya wakina dada wenye tabia ya kuwategeshea wanaume zao ili wapate watoto kwa kuwaambia hicho wanachokifanya hakina utofauti na unyanyasaji hivyo wanapaswa wabadilike katika hilo jambo.

Fid Q ameeleza hayo kupitia tinga namba moja kwa vijana EATV katika kipindi cha eNewz baada ya kuwepo wimbi kubwa la wanaume kukataa kulea watoto  wao kwa kisingizio cha kusema hakuwa wamejiandaa katika kipindi hicho kuwa walezi wa mtoto.

"Huo ni ukatili na dhuruma, ongea na mtu mkubaliane na siyo umtegeshee mwenzako ili upate mtoto. Maisha siku hizi ni magumu sana, watu wanaishi kwa mipango na ratiba kamili ya mwaka kwa lugha nyepesi naweza sema watu wanaishi kwa 'principal'. Kwa hiyo ushauri wangu kwa wakina dada acheni ukatili na mjitahidi kuongea na wenza wenu ili muweze kupata kile mnachostahili katika mahusiani yenu", amesema Fid Q.

Mbali na hilo, Fid Q amedai hata kama umri wake unazidi kusogea mbele na kuwa mzee hayupo tayari kukurupuka kuingia katika ndoa.

"Siyo kitu cha kukimbilia maana wanasemaga bora ukosee kazi kuliko kukosea mke wa kuoa, kwa sababu ukikosea kuchagua mke wa kuoa anaweza kukuharibia maisha yako yote. Kwa hiyo tayari nina 'idea' na mtu ambaye anafaa kuolewa na mimi chamsingi tu nawaomba mniombee dua za kheri, ili nasi tuone kama tutaweza kutimiza moja ya suna kubwa za binadamu", amesisitiza Fid Q.