SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 8 Septemba 2017

T media news

Chelsea, Arsenal, Liverpool zatofautiana na Man City na United katika suala la usajili


Kulikuwepo mjadala wa muda sasa kuhusu muda sahihi wa kufungwa kwa dirisha la usajili katika ligi kuu ya Uingereza Epl, kila klabu ilikuwa na mtazamo wake kuhusu muda wa kufungwa kwa dirisha hilo.

Kwa kawaida dirisha la usajili la Epl hufungwa mwezi wa nane mwisho wakati ambao ligi kuu nchini Uingereza inakuwa tayari inaendelea na mechi zainakuwa zimeshaanza kupigwa.

Baadhi ya timu ikiwemo Arsenal zilidai suala hilo halipaswi kuwa hivyo na inapaswa kwa dirisha hilo kufungwa wakati ligi ikiwa bado haijaanza huku vilabu kama Watford vikitaka muda uwe hivyo hivyo.

Shirikisho la soka la nchini Uingereza likaona vilabu vipige kura ili kuamua suala hilo na kura nyingi zitakavyokuwa ndio muda wa dirisha la usajili utaaamriwa na kura zikapigwa kuamua dirisha la usajili libadilishwe muda ua laa.

Jana ndio siku ambayo zilipigwa kura ambapo vilabu 14 ikiwemo Arsenal, Chelsea, Liverpool, Tottenham walipiga kura ya ndio, kwamba dirisha hilo liwe linafungwa mapema kabla ligi kuu ya Uingereza haijaaanza.

Lakini majirani wawili mahasimu kutoka jiji la Manchester wao walisema hapana wakimaanisha kwamba muda wa dirisha hilo la usajili kufungwa uwe huu huu unaotumika siku zote ambapo huwa linafungwa huku ligi ikiwa imeanza.

Sio Man United tu na City wanaotaka lifungwe huku ligi ikiwa imeanza bali pia Watford, Swansea, Crystal Palace pia waliungana na City na United huku Burnley wakiwa hawajapiga kura kabisa.