SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 26 Septemba 2017

T media news

BUNDA:Naibu Waziri wa Afya ameanza awamu nyingine ya ziara ya kuimarisha mfumo wa afya nchini. Ameanzia mkoani Mara, Wilaya ya Bunda.

Hapa ni Zahanati ya Kijiji cha Sanzate, Wilayani Bunda.

Wananchi wa hapa na Mbunge wao, Mhe. Boniface Mwita Getere (Mb.) wana kiu kubwa ya kutaka Zahanati yao waliyoanza kuijenga mwaka 2001, leo zaidi ya miaka 16, ifunguliwe. Wamechoka kufuata huduma za afya KM 20 toka kijijini kwao kwenda Mugeta, kilipo Kituo cha afya cha jirani zaidi.

Mwaka jana tulipopita hapa waliomba tusaidie kituo hiki kifunguliwe. Tulishindwa sababu kulikuwa na mapungufu kadhaa. Nikawaelekeza mambo kadhaa ya kufanyia kazi kabla hatujakifungua, yakiwemo kujenga Incinerator (ya kuteketezea taka hatarishi), shimo maalum la kuteketezea kondo la nyuma la uzazi (placenta pit), Choo, nyumba ya watumishi na finishing ya jengo lenyewe la zahanati. Sehemu kubwa wametekeleza.

Huyu mzee is a proud man today, pia ana matumaini makubwa sana, ananionesha namna walivyofanikisha utekelezaji wa agizo letu, anajiamini sana kuwa leo tutatamka kuifungua rasmi.

Wananchi wakiwa na maslahi na mradi wao huwa wanajituma sana. Hii 'ownership' ya mradi ni kielelezo cha umuhimu wa huduma zenyewe na uhitaji wake mbele ya macho ya wananchi.

Tumewapa Halmashauri miezi mitatu waweke sawa mambo yao kisha Zahanati hii ifunguliwe.

 #HK #ImarishaAfya #AgizoLaMwandoya #StrengtheningHealthSystems #Bunda #Mara #MzeeWaField #SiasaNiVitendo #HamisiKigwangalla