SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumapili, 17 Septemba 2017

T media news

Brazil yaisamehe Tanzania deni la Mabilioni la mwaka 1979

Serikali Brazil imeisamehe Tanzania deni la jumla ya Dola za Kimarekani Mil. 203 ambazo ni sawa na Tsh Bil. 455 ambapo deni hilo lilitokana na mkopo uliotolewa kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Morogoro-Dodoma mwaka 1979 pamoja riba.

Balozi wa Tanzania Nchini Brazil, Dk Emmanuel Nchimbi ameishukuru Serikali ya Brazil kwa msamaha huo ambao amesema imeunga mkono jitihada za Rais Dk. John Magufuli kujenga uchumi imara wa Tanzania.

Tunaishukuru Serikali ya Brazil kwa kuunga mkono jitihada za Rais Dkt Magufuli za kujenga uchumi imara wa Tanzania, alisema Balozi Nchimbi.

Kwa upande wa afisa wa Brazil amesema,“tumefungua rasmi milango ya ushirikiano wa kifedha na kibiashara iliyokuwa imefungwa kutokana na Deni hilo.”

Kufuatia hatua hiyo, Makampuni ya Brazil yataruhusiwa kukopa katika Benki za Brazil kwa ajili ya kutekeleza miradi nchini Tanzania, pia Serikali ya Tanzania inaruhusiwa rasmi kuanzisha majadiliano ya miradi mipya ya maendeleo na Brazil.