SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 11 Septemba 2017

T media news

Arsenal na Espanyol waongoza orodha ya vibonde kwa wikeindi iliyopita

Sasa tunasubiri Champions League ambayo kuanzia kesho itaanza kupigwa, lakini wikiendi hii kulikuwa na michezo ya ligi mbali mbali iliyopigwa dunia nzima kuanzia Tanzania hadi Ulaya.

Mambo mengi yametokeoa katika michezo hiyo Lukaku amefikisha mabao 150, Mourinho amekataa kupeana mkono na Mark Hughes, Lioneil Messi amepiga hattrick yake nyingine katika ligi kuu La Liga.


Lakini sahau ayo yote bali kuna timu ambazo zilipokea vipigo vikubwa sana, Arsenal anaongoza kwani kipigo cha bao 5 kwa 0 toka kwa Man City kilikuwa kipigo kikubwa zaidi katika ligi zinazopendwa barani Ulaya.

Sio tu Arsenal bali nao pia wana vibonde wao, Espanyol. Wahispania hawa sawa na Arsenal walichezea bao 5 kwa 0 toka kwa Barcelona na kuwafanya nao kuingia katika orodha ya vibonde wa ligi.

Mabingwa watetezi wa Ufaransa As Monaco nao almanusra waaibike baada ya Nice waliokuwa wakaiongozwa na Mario Balotelli kuwachapa bao 4 kwa 0 huku Balotelli akifunga mara mbili.

Bado mipambano hii inaendelea na ni wazi kwamba tutazidi kuona vipigo vikubwa zaidi katika ligi hizi kutokana na uchu wa washambuliaji katika kupachika mabao.