SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 15 Agosti 2017

T media news

Uwoya Apewa Mwaliko na Jaguar Kushuhudia Kuapishwa kwa Kenyatta

Msanii wa filamu za kibongo Irene Uwoya ambaye hivi karibuni amekuwa gumzo baada ya sakata la ndoa yake kuwekwa wazi na mumewe Hamad Ndikumana huku akimtuhumu kuwahi kuwa na mahusiano na msanii kutoka Kenya Jaguar.

Hivi karibuni msanii Jaguar ameshinda ubunge wa jimbo la Starehe kwenye uchaguzi mkuu nchini Kenya, na kukawa na tetesi kwamba Irene Uwoya amealikwa kushuhudia kuapishwa kwa Rais Uhuru Kenyata huku mualiko huo ukitolewa na Jaguar.

Akizungumza na mwandishi wetu Irene Uwoya amekiri kupewa mualiko huo na kusema kama atapata nafasi atahudhuria sherehe hizo, lakini aligoma kufunguka kama kweli ana mahusiano na msanii Jaguar.

"Kwanza huwa sipendi masuala ya mahusiano yangu kuweka wazi kwenye vyombo vya habari, na kuhusu kwenda Kenya nikapata nafasi nitahudhuria nimepewa mualiko, lakini kwa sasa nashoot hivyo nikipata nafasi nitahudhuria", alisema Irene Uwoya.
Sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa Kenya Uhuru Kenyata zinatarajiwa kufanyika tarehe 29 mwezi huu nchini Kenya, zitakazohudhuriwa na mamia ya wananchi wa Kenya.