Katika jambo hili kuna hoja au issues zifuatazo
1. *Je, TANROADS wana mamlaka ya kupiga faini kwa kosa la mwendokasi?*
*JIBU*
TANROADS kama mamlaka ya usimamizi wa barabara chini ya Sheria ya barabara (ROADS ACT 2007) inayo mamlaka ya kuwaadhibu wale wote wanaokiuka mwendo uliooneshwa kwenye alama za barabarani au kadiri ya maelekezo yao.
Mamlaka haya wanayapata kwa mujibu wa kifungu cha 32(2) cha Sheria ya barabara. Hata hivyo, ili mtu atozwe faini chini ya sheria hiyo ni hadi atiwe hatiani.
Inayotia mtu hatiani ni mahakama. Hivyo ukikamatwa na TANROADS unatakiwa kufikishwa mahakamani na huko ukipatikana na hatia uweze kutozwa kiasi cha shilingi 200.000 au jela mwaka 1, na sio vinginevyo.
2. *Ikiwa jibu ni NDIYO, ni kwa sheria gani na kifungu gani?*
*JIBU*: Kifungu cha 32(2) cha sheria ya Barabara, Na.13 ya mwaka 2007
3. *Je ni kweli faini za barabarani kwa kosa la mwendokasi sasa ni sh 200.000 na inagawanyika mara tatu yaani kiasi cha shilingi 90000 kinaenda TANROADS, Kiasi kinaenda 80000 kinaenda SUMATRA na kinachobaki TRAFIKI?*
*JIBU* ni HAPANA.
Huu ni upotoshaji. Faini ya chini ya sheria ya barabara ni shilingi 200000 kwa kuzidisha mwendo kinyume na kifungu cha 32(2) na haigawanyiki.
4. *Je, inawezejana mtu mmoja akaadhibiwa na mamlaka zote tatu kwa pamoja?* Yaani mfano kapigwa tochi na TANROADS kwa kuzidisha mwendo TANROADS wakamwandikia 200,000; SUMATRA nao wakamwandikia 200,000 na Trafiki nao wakamwandikia 30,000??(tuchukulie mamlaka zote 3 zipo barabarani kwa wakati mmoja eneo moja zinafanya operesheni)
*JIBU* ni HAPANA.
Haiwezekani kutozwa faini zaidi ya moja kwa kosa hilo hilo. Kwani sheria inasema *Mtu hataadhibiwa mara mbili kwa kosa hilo hilo alilolitenda mara moja*. Iwapo mtu ameadhibiwa mara mbili adhabu hiyo ya pili ni batili.
Ndio kusema kwamba hata mamlaka zote 3 ziwepo pamoja, ukakamatwa umezidisha mwendo utaadhibiwa mara moja tu na mamlaka ile iliyokukamata.
5. *Nini kimepelekea kuwepo sheria 3 kwa jambo hilo hilo moja?*
*JIBU*
Kila sheria imetungwa kipindi tofauti na nyingine na kila sheria inasimamiwa na mamlaka yake bila mamlaka moja kuiingilia nyingine.
SUMATRA anasimamia Transport licensing Act Cap 317 na kanuni zake, ambapo faini ni kati ya shilingi 200000 na 500000;
TANROADS anasimamia ROADS ACT 2007 pamoja na kanuni zake za mwaka 2009, ambapo faini ni shilingi 200.000;
POLISI anaisimamia ROAD TRAFFIC ACT Cap 168 ambapo faini yake ya papo kwa papo ni shilingi 30000 bila kujali ukubwa au udogo wa kosa.
6. *Je, Polisi akikukamata anaweza kukuandikia faini kwa kutumia sheria ya TANROADS au SUMATRA?*
*JIBU* ni HAPANA.
Askari anatakiwa kukuandikia faini kwa mujibu wa sheria ya usalama barabarani yaani ROAD TRAFFIC ACT. Kama atataka uandikiwe faini na mamlaka hizo nyingine itabidi akukabidhishe huko ili utendewe kwa mujibuwa sheria hizo.
Ni matumaini yetu kuwa kw maswali na majibu haya utakuwa umeongeza uelewa wako kuhusu faini za mwendokasi barabarani kwa mamlaka zote tatu.
Kazi yetu ni kukuelimisha.
RSA TANZANIA.
USALAMA BARABARANI NI JUKUMU LETU SOTE.
Share na mwenzio.
