SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 15 Agosti 2017

T media news

Moto wa Ajabu Wazua Taharuki Kwa Wakazi wa Kitunda.....

Moto wa ajabu unadaiwa kutokea katika nyumba moja iliyopo maeneo ya Kitunda jijini Dar es salaam na kusababisha taharuki kwa wakazi wa eneo hilo.

Kupitia kipindi cha Leo Tena ya Clouds Fm inadaiwa kuwa moto huo umekuwa ukiwaka kimaajabu katika maeneo tofauti katika nyumba hiyo ikiwemo chumbani na kupelekea kuharibu baadhi ya vitu uikiwemo nguo, na kusababisha wakazi wa nyumba hiyo kushindwa kulala.

Mwanamke wa nyumba hiyo aliyefahamika kwa jina la Mama Vicent ameeleza kuwa moto huo umekuwa ukiwaka kimazingira tofauti na kupelekea kuunguza sehemu hizo ikiwemo dirishani hadi kumaliza madirisha hayo licha ya kufanikiwa kuuzima.

Hata hivyo ameongeza kuwa aliporudi mumewe alimwambia lakini kesho yake ikatokea tena ambapo moto uliwaka katika moja ya kochi lao na kisha kuhamia katika makochi mengine na baadae moto huo ukahamia katika chumbani.

“Moto umekuwa unawaka mara kwa mara ikapelekea majirani kuhamia hapa nyumbani, mimi nikawa nalia nasema jamani ni fulani huyo kwa nini anaiambie hivyo, mkewe akawa anatoka anaenda kumwambia  mumewe kuwa nimemtaja mara moto huo unawaka,”amesema mwanamke huyo.

Pia ameongeza kuwa baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya ikabidi kuita wachungaji wa kanisani nyumbani kwake na kuombea nyumba hiyo ambayo imeteketea kwa moto pamoja na vitu ikaacha kuwaka moto.