SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 7 Agosti 2017

T media news

Kuelekea mchezo wa Madrid vs Man Utd, hizi ndio takwimu na rekodi za UEFA Super Cup

Msimu mpya wa soka barani unatarajiwa kuanza rasmi kesho wakati utakapopigwa mtanange utakaowakutanisha wababe wa ulaya msimu uliopita. Mabingwa wa Champions League Real Madrid na mabingwa wa Europa Cup Manchester United.

Mchezo huu utapigwa nchini Macedonia 🇲🇰 mashariki mwa bara la ulaya, kuanzia majira ya 9:45 usiku.
Mchezo huu unakutanisha miamba mikubwa ya soka barani ulaya siku chache baada ya kukutana nchini Marekani katika mechi za maandalizi ya msimu mpya. 
Cristiano Ronaldo amerejea mazoezini wiki iliyopita na leo ametajwa katika kikosi kinachosafiro kuelekea Macedonia kwa ajili ya mchezo huo, United watamkosa Eric Bailly pamoja na Phil Jones wenye adhabu za kufungiwa mechi kutokana na makosa ambayo waliyatenda msimu uliopita.

Kwa kuanzia kuuchambua mchezo huu tuanze kuangalia takwimu mbalimbali zinazohusisha mchezo wa UEFA Super Cup tangu ulipoanzishwa kuchezwa mnamo mwaka 1973.

Champions League vs UEFA Cup Winners

Mabingwa wa Champions League wameshinda kombe hili mara 22 kati ya mara 41.

Mabingwa wa UEFA Cup/UEFA Europa League wameshinda kombe hili mara 7 kati ya 17 tangu lilipokufa kombe la Washindi (UEFA Cup Winners' Cup.)

Mataifa yaliyoshinda mara nyingi
13: Spain 🇪🇸 wameshinda kombe hili mara 13 kupitia vilabu vyao (Barcelona 5, Real Madrid 3, Valencia 2, Atlético Madrid 2, Sevilla 1)

9: Italy 🇮🇹 wameshinda Super Cup mara 9 kupitia vilabu vyao (AC Milan 5, Juventus 2, Lazio 1, Parma 1)

7: England wanafuatia kwa kushinda mara 7 (Liverpool 3, Aston Villa 1, Chelsea 1, Manchester United 1, Nottingham Forest 1)

Vilabu vilivyoshinda UEFA Super Cup mara nyingi 
5: AC Milan, Barcelona
3: Liverpool, Real Madrid
2: Ajax, Anderlecht, Atlético Madrid, Juventus, Valencia

Mchezaji aliyeshinda Super Cup Mara nyingi 
4= Dani Alves (Sevilla 2006, Barcelona 2009,20112015)
4= Paolo Maldini (AC Milan 198919901994,2003)

Kocha aliyeshinda mara nyingi
3= Carlo Ancelotti (AC Milan 20032007, Real Madrid 2014)
3= Josep Guardiola (Barcelona 20092011, Bayern München 2013)

Nchi zilizoshiriki mchezo wa Super Cup mara nyingi 
25: Spain 🇪🇸 wameshiriki mara 25 kupitia vilabu vya (Barcelona 9, Real Madrid 6, Sevilla 5, Valencia 2, Atlético Madrid 2, Real Zaragoza 1)

16: Waingereza 🇬🇧 wameshiriki mara 16 kupitia vilabu vya (Liverpool 5, Manchester United 4, Chelsea 3, Nottingham Forest 2, Arsenal 1, Aston Villa 1)

13: Italy 🇮🇹 mara 13 (AC Milan 7, Juventus 2, Internazionale Milano 1, Parma 1, Lazio 1, Sampdoria 1)


Vilabu vilivyoshiriki mara nyingi 
9: Barcelona
7: AC Milan
6: Real Madrid
5: Liverpool, Sevilla
4: Bayern München, Porto, Manchester United

Mchezo uliokuwa na idadi kubwa ya magoli : 2015, Barcelona 5-4 Sevilla

Ushindi mkubwa zaidi *: 2006, Sevilla 3-0 Barcelona, na mtanange wa 2012 kati ya Atlético Madrid 4-1 Chelsea

Rekodi binafsi

Goli la haraka zaidi: Éver Banega (Dakika 3
2015: Barcelona 5-4 Sevilla)

Waliofunga Hat-tricks: Radamel Falcao (2012, Atlético Madrid v Chelsea) na Terry McDermott (1977, Liverpool v Hamburg)

Waliofunga magoli ya kujifunga: Patrick Paauwe alijifunga goli pekee katika historia ya Super Cup kwenye mchezo wa kipigo cha Feyenoord cha mabao 3-1 kutoka kwa Real Madrid mwaka 2002.

Waliopata kadi nyekundu: Wachezaji wanne wameshapata kadi nyekundu kwenye mchezo wa Super Cup
 Paul Scholes (2008, United), Rolando na Fredy Guarín (2011, Porto) na Thimothée Kolodziejczak (Sevilla, 2016).

Wachezaji waliocheza mechi nyingi za UEFA Super Cup **
8: Alessandro Costacurta (AC Milan), Roberto Donadoni (AC Milan)
7: Paolo Maldini (AC Milan), Daniele Massaro (AC Milan), Mauro Tassotti (AC Milan)
6: Franco Baresi (AC Milan), Arie Haan (Ajax, Anderlecht)
5: Dani Alves (Sevilla, Barcelona), Marcel Desailly (AC Milan, Chelsea), Albert Ferrer (Barcelona, Chelsea), Ronald Koeman (PSV Eindhoven, Barcelona), Attilio Lombardo (Sampdoria, Juventus, Lazio), Phil Neal (Liverpool)

Wafungaji bora wa UEFA Super Cup 
3: Oleh Blokhin (Dynamo Kyiv), Radamel Falcao (Atlético Madrid), Arie Haan (Ajax, Anderlecht), Terry McDermott (Liverpool), Lionel Messi (Barcelona), Gerd Müller (Bayern München), Rob Rensenbrink (Anderlecht), François Van der Elst (Anderlecht

**UEFA Super Cup ulikuwa unachezwa kwa mfumo wa mechi za nyumbani na ugenini kuanzia mwaka 1973 mpaka 1997.