Baada ya kuripoti habari ya mwanamke mmoja kupigwa na polisi, Hatimae Mbunge wa jimbo la bunda mji amejitolea kulipa garama zote za matibabu anazodaiwa mgonjwa huyo aliyelazwa katika zahanati ya Bhoke.
Mbunge wa jimbo la Bunda Mjini Mh Ester Amos Bulaya leo amemtembelea na kumuona mgonjwa Christina Machera aliyelazwa katika Dispensary ya Bhoke mjini hapa kufutiatia kupatwa na ugonjwa wa malaria pamoja na matatizo ya kubwana kifua, yaliyomkabili zaidi alipokamatwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kuchelewa kufunga baa yake na kufikishwa kituoni siku ya jumanne.
Akizungumza na waandishi wa habari katika dispensary hiyo Mheshimiwa Bulaya amesema kuwa atamlipia garama zote za matibabu Christina machera, huku akishangazwa na madai ya jeshi hilo kumshambulia mama huyo.
Amesema jeshi la polisi hivi karibuni amelipongeza kwa utendaji wao mzuri katika shughuli zao za ulinzi wa raia na mali zao lakini wachache wanaweza kuharibu taswira hiyo kwa kukiuka sheria na taratibu za kazi zao.
Mbunge huyo amesema kuwa yeye ni mtu wa usawa na ukizingatia tatizo hilo limemkuta mwanamke hivyo atalifuatilia na halitaishia hapo.
Naye mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Bunda Mwl Lydia Bupilipili amekiambia kituo hiki mchana wa leo kuwa Bi Christina hakupigwa na polisi kiasi cha kupelekea kudhoofikia badala yake alikuwa akisumbuliwa na kifua kikuu pamoja na Maleria na kuongeza kuwa hata taarifa za hospitali zinaonyesha kuwa alikuwa akipatiwa matibabu mara kwa mara kwa maradhi ya kifua kikuu.
Aidha uongozi wa Bhoke Dispensary imeeleza kuwa mgonjwa huyo anaendelea vizuri na muda wowote ataruhusiwa kurudi nyumbani.
