Bunda
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Christina Machere amedai kuwa amepigwa na askari wa Jeshi la Polisi Mjini Bunda Mkoa wa Mara kwa madai ya kuchelewa kufunga ofisi yake ya biahara ya kuuza pombe aina ya bia.
Ameeleza kuwa askari hao wamemuonea kufuatia hatua walioichukua dhidi yake ya kumpiga kwakuwa alikuwa hafadnyi biashara badala yake alikuwa akisubiria dereva pikipiki kwa ajili ya kumpeleka nyumba kwani hali yake haikuwa nzuri.
Amesema kwake na eneo lake la kazi sio mbali, na ni sehemu ambayo mara zote amekuwa akienda kwa miguu baada ya kufanya biashara yake lakini kutokana na hali yake kiafya kuwa mbaya aliamua kusubiri pikipika kwa ajili ya kumuwaisha nyumbani na ndipo askari hao wakamkuta katika eneo hilo na kasha kumkamata huku wengine wakimpiga kifua na kumpeleka kituoni.
Baada ya kumpeleka kituani bi Christina aliwaeleza askari hao kuwa anajiskia vibaya lakini hawakumuelewa hadi hali yake ikadhoofu zaidi ndipo wakaamua kuita gari la polisi na kumpokea zahanati ya Boke iliyoko mtaa wa benki majira ya saa nane usiku na kwa matibabu zaidi.
Aidha uongozi wa zahanati hiyo imekiri kumpokea mgonjwa huyo lakini wameeleza kuwa walimpokea kama wagonjwa wengine na sio kama mgonjwa aliekuwa na majeraha ya kupigwa kwakuwa hakuwa na PF 3 Kutoka jeshi la polisi.
Uongozi wa zahanati hiyo umeeleza kuwa baada ya kupimwa aligundulika kusumbuliwa na maumivu ya kifua na kubainika kuwa maumivu hayo yalikuwa yanatokana na ugonjwa wa malaria.
Aidha redio mazingira ilipomtafuta kamanda wa polisi Mkoa wa Mara Jafari Mohamed kuthibitisha taarifa hizo simu yake ilikuwa ikiita pasina kupokelewa .
Naye mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Bunda Lydia Bupilipili alipotafutwa kwa njia ya simu kujua kama anajua taarifa kuhusu tukio hilo akajibu kwa njia ya ujumbe mfupi kuwa tumpe muda aulize na kufuatilia.
Aidha redio mazingira fm ilifuatilia kujua kwa wafanyabishara kuhusu tukio hilo kama wanalifahamu lakini wengi wao walikuwa wakiogopa kuliongelea huku wangine wakikiri kulifahamu pasina kukubali kuchukuliwa sauti ingawa waliongelea muda wa kufanya biashara nyakati za usiku huku baadhi yao wakieleza kuwa wapo baadhi yao wanaofanya biashara hadi muda usioruhusiwa kisheria kwa kukaa na wateja wao ndani na kuwafungia mlango huku wakiendelea kunywa pombe.