ARUSHA: Wamiliki wa Shule Binafsi pamoja na Meya wa Jiji la Arusha waliokuwa wameongozana na waandishi wa habari kwenda kutoa rambirambi katika Shule ya Msingi Lucky Vicent, wamewekwa chini ya ulinzi na Jeshi la Polisi wakituhumiwa kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria shuleni hapo.
Wamiliki hao walikuwa wameongozana pia na baadhi ya viongozi wa dini pamoja na baadhi ya wazazi waliofiwa na watoto wao katika ajali iliyotokea huko Rhotia, wilaya ya Karatu, mkoani Aursha.