Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeendelea na zoezi la uhamasishaji wa Ulipaji wa Kodi ya Pango la Ardhi nchini.
Wamiliki wa Ardhi wameendelea kujitokeza katika kufanya malipo yao nchini kote.
Hatahivyo, Wizara inaendelea kuwakumbusha wale wote wanao miliki viwanja na mashamba yaliyopimwa, ambao bado hawajalipa Kodi ya Pango la Ardhi, wahusike kufanya malipo hayo kabla ya mwisho wa mwezi wa sita (6), kwani Ifikapo tarehe 30/06hatua zifuatazo zitachukuliwa dhidi yao;Watashitakiwa Mahakamani, Mali zao zitakamatwa na majengo yao kupigwa mnada kwa kupitia madalali na Miliki zao zitafutwa.
Aidha, hatua zote zitakazochukuliwa dhidi yao zitakuwa kwa mujibu wa Sheria. (Sheria ya Ardhi Na. 4 ya mwaka 1999, katika vifungu Na. 49 – 50).
Mwananchi Lipa Kodi ya Pango la Ardhi kwa Maendeleo ya Taifa Letu.
Wamiliki wa Viwanja na Mashamba wakiendelea kujitokeza kufanya malipo ya Kodi ya Pango la Ardhi katika kituo cha malipo cha Ardhi Street – Kivukoni
Watumishi wa Kitengo cha Kodi wakiwa Mkoani Arusha katika zoezi la kusambaza Hati za madai.
Mkuu wa Kitengo cha Kodi; Dennis Masami akielimisha Umma kuhusu Ulipaji wa Kodi ya Pango la Ardhi kupitia Televisheni /Azam TV katika kipindi cha Morning Trumpet.
Mkuu wa Kitengo cha Kodi; Dennis Masami akielimisha Umma kuhusu Ulipaji wa Kodi ya Pango la Ardhi kupitia Radio/Radio Times FM katika kipindi cha Dira Yetu