SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 17 Mei 2017

T media news

UKWELI Mchungu..Hili ni Taifa la Wanung'unikao Mno: Tulideka, Tulidekezwa, au Tulidekeka..!!!?


Swali Korofishi: Hivi sisi kama taifa ni kuwa tulikuwa tumedekezwa, tumedeka au tumedekeka mno? Maana, kuna baadhi ya mambo yanapotokea hadi unashangaa tulikuwa ni watu wa aina gani? Sukari imebadilika bei kidogo, "mamaaa wee tunakufa sukari imepanda bei!" utadhani sukari inatakiwa iwe kwenye bei ile ile ya miaka kumi iliyopita! Mara upungufu kidogo wa chakula baadhi ya maeneo "Mamamaaa wewee tunakufa njaaa, watu wanakufa njaa"!

Kigogo kapigwa mkwara na imechomolewa bastola - wala hajalengwa mtu wala nini - "mama weweeeeee watu wanatumia bastola, n.k!" Hivi tulijenga taifa la namna gani? Yaani, tunaonekana kukereka na vitu vidogo na wakati mwingine vya kawaida sana (hata kama ni vikubwa) hadi inashangaza.

TUlizoea kuona vigogo wanaweza kufanya lolote au popote na kwa mtu yeyote, leo watu wanaoneshwa kuwa sheria haina macho watu tunaanza kushangaa "eeh wamemfanyia hivi na yule" wakati miaka yote tulitaka tuone sheria zinatumika sawasawa bila kujali nani ni nani. Mwisho watu wanasema "wataisoma namba". Si tulitaka tuone kuwa wana CCM nao wanatendewa vile vile wanavyotendewa wengine? Sasa leo wanatendewa tunashangaa? si ndio maana ya sheria?

Hivi tukianza kuona sheria inauma ikienda na kurudi tunashangaa?NI taifa la watu wasio taka kupata shida hata kidogo sisi? Hivi tungekuwa katika mazingira ya watu wa nchi nyingine ingekuwaje? Nakumbuka kuna watu walikuwa wanataka hata "jeshi lichukue" nchi! Hivi kweli walikuwa wanamaanisha au walidhani ikitokea itakuwa ni kusimama na kuimba "kumbaiya my Lord kumbaiya"?

Jamani, mabadiliko yoyote yale ni magumu. Lakini pia kama watu wanaona hivi sivyo wanavyotaka njia pekee ni kujipanga na kuanza kujiandaa kubadilisha mwelekeo wa nchi katika uchaguzi ujao. Na kama mambo ni magumu kweli basi ni jukumuu la watu kuanza kuamua sasa hivi wanataka iweje; si wameona yanayotokea Venezuela?

Maana imefikia watu wanatamana kurudi wakati wa Kikwete na Mkapa! Inashangaza sana!