SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 18 Mei 2017

T media news

Maskini Pogba awatoa machozi mashabiki wake.

Wiki iliyopita habari mbaya kwa mchezeaji Paul Pogna ni kifo cha baba yake mzazi mzee Fassou Antoine, mzee huyo alifariki dunia baada ya maradhi yaliyomsumbua kwa muda mrefu.

Pogba tayari yuko Ufaransa kwa ajili ya mazishi ya baba yake na hakuwepo katika mchezo wa United dhidi ya Tottenham huku pia akikosa mchezo kati ya United dhidi ya Southampton.

Pogba kupitia ukurasa wake wa Instagram aliweka video ambayo inamuonesha akiwa na baba yake siku za mwisho mwisho za uhai wake huku wakitaniana na wakionekana wenye furaha.

Katika video hiyo Pogba alionekana akijaribu kumfundisha baba yake jinsi ya “kudab” staili ambayo Pogba amekuwa akiitumia mara nyingi akiwa anashangilia mabao yake.

Video hiyo imeamsha hisia za huzuni kwa mashabiki wa mchezaji huyo na huku akiandika maneno ya kuzishukuru hospitali zote na madaktari waliojaribu kupigania afya ya mzazi wake.

Ni wazi kwamba kutokana na msiba huo sasa Paul Pogba atakuwa nje ya uwanja hadi wakati wa fainali ya michuano ya Europa ambayo itapigwa tarehe 24 nchini Sweden.