SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 18 Mei 2017

T media news

Kuelekea Serengeti Boys vs Angola, hii ni ripoti ya Doctor na mipango ya kocha

Leo Mei 18, 2017 Serengeti Boys inatupa karata yake ya pili dhidi ya Angola kwenye michuano ya AFCON U17 inayoendelea nchini Gabon.

Mchezo huu ni muhimu kwa Serengeti Boys kupata matokeo ya ushindi ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo lakini pia kukata tiketi ya kucheza kombe la dunia kwa vijana baadae mwaka huu huko nchini India.

Kikosi cha Serengeti Boys jana kilifanya mazoezi yake ya mwisho huku wachezaji wote wakishiriki mazoezi hayo kasoro Ally Makamba ambae alipata majeraha makubwa ya mguu kabla ya mashindano lakini inaelezwa anaendelea vizuri na matibabu.

Kwenye mchezo dhidi ya Mali kuna baadi ya wachezaji walishindwa kuendelea na mazoezi baada ya kupata majereha, daktari mkuu wa timu anasema wote wanaendelea vizuri.

“Wote wanaendelea vizuri wengine ilikuwa ni matatizo ya misuli lakini tulivyoanza kuwapa matibabu walipata nafuu na yule ambae alipata matatizo kwenye kichwa anaendelea vizuri”

“Wachezaji wana morali ya hali ya juu halafu wachezaji walikua hawajaelezwa nini maana ya fair play lakini tayari wameshaambiwa kuhusu spiri ya fair play na sisi jopo la tiba tumewaelekeza mbinu za kukwepa adui anaekuja kwa uhatarishi.”

Kwa upande wa kocha mkuu wa Serengeti Boys Bakari Shime yeye ameeleza mipango kuelekea mchezo dhidi ya Angola ukizingatia walitoka suluhu kwenye mechi yao ya ufunguzi dhidi ya Mali.

“Mchezo dhidi ya Angola ni muhimu sana kwetu na tunajua endapo tutashinda tunatengeneza asilimia 80 ya kufuzu hatua ya nusu fainali, kimsingi tumejiandaa kwa hilo.”

“Tulikua na plan A dhidi ya Mali kwa kuwa tulikua hatuwafahamu tukatumia muda mwingi kujilinda ili kupata alama moja kwa ajili ya kuanza mashindano haya na tayari tumepata.”

“Mchezo dhidi ya Angola unaeleke kuamua hatima yetu na tumejipanga kushambulia huku tukiwa makini katika kujilinda, kwa hiyo watanzania watashuhudia mpira waliozoea kuuona tukicheza.”

Mechi kati ya Serengeti Boys dhidi ya Angola utaanza saa 9:30 alasiri kwa saa za Gabon sawa na saa 11:30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.