SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 18 Mei 2017

T media news

Kiongozi mwingine wa CCM auawa usiku wa kuamkia leo Kibiti


Katika hali inayoendelea kushangaza dhidi ya mtukio ya mauaji mkoani Pwani, usiku wa kuamkia leo, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tawi la Njia Nne, Iddy Kirungi liliopo katika kijiji cha Muyuyu, Kata ya Mtunda wilayani  Kibiti ameuawa kwa kupigwa risasi akiwa kwake.

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Juma Njwayo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Rufiji amethibitisha kutokea mauaji hayo na kusema marehemu alipigwa risasi akiwa kwake wakati akijaribu kukimbia.

Njwayo amesema kabla ya kuuawa kwa mwenyekiti huyo, pia wauaji hao walianza kumjeruhi kwa kumpiga risasi ya tumboni mtoto wa marehemu aliyetajwa kwa jina la Nurdin Iddy Kirungi.

Mganga wa zamu katika Kituo cha Afya Ikwiriri, Dk Rashid Omar alisema walimpokea Nurdin akiwa na jeraha kubwa tumboni mwake ambalo halikutokeza upande wa pili.

Alisema majeruhi huyo walimpatia rufaa kwenda Hospital ya Mchukwi kutokana na kuwa anavuja damu nyingi sana.