SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 25 Mei 2017

T media news

HABARI NA HISTORIA YA TANU NA UKOMBOZI WA TANZANIA: MISUKOSUKO NA MABALAA DAR ES SALAAM


SEHEMU YA KWANZA.
Hakika katika historia ya Tanzania hasa kwa upande wa ukombozi hatuwezi kuacha kuzungumzia chama cha ukombozi cha TANU. Chama hiki kina historia ndefu kwa kiasi Fulani.kwa ufupi sana, Chimbuko la chama cha TANU (Tanzania African National Union) Lilianzia miaka ya 1910-1920 ambapo kulianzishwa chama cha Wafanyakazi mnamo mwanzoni mwa miaka ya 1920 kilichofahamika kama Tanganyika African Civil Service Association (TSGA).Na mnamo mwaka 1929 kikaundwa chama cha TAA( Tanganyika African Association) jijini Dar es Salaam. Na mpaka kufikia mwaka 1954 chama cha TANU (Tanzania African National Union) kiliundwa na Mwalimu Nyerere alikuwa mwenyekiti. Na mara baada ya Uhuru mnamo mwaka 1961, yaani miaka ya 1977 chama cha TANU kilibadilishwa na kuwa  CCM(Chama Cha Mapinduzi) jijini Dar Es Salaam.

Na mara baada ya kufahamu historia  fupi, turudi kwenye misukosuko waliokuwa wakiipata mapigamia Uhuru wa Tanzania wakiwa kwenye chama cha TANU. Ukweli ni kwamba wakati wa kupigania Uhuru kulikuwa na mambo mengi sana yaliokuwa yakiwakumba wapigania uhuru. Licha ya kwamba Tanganyika ilipata Uhuru wake kwa njia ya Amani, bado wapigania Uhuru walipata shida sana na pengine kama wasingekuwa na umoja na kutokukata tamaa tusingepata uhuru miaka iliotajwa hapo juu. Hivyo Tuanze kufahamu misukosuko na mabalaa jijini Dar es Salaam ambapo vuguvugu la kupigania uhuru lilipoanzia. Kwanza kulikuwa na misukosuko ya baadhi ya wasomi waliokuwa wameshiba elimu ya mkoloni  na kuwafanya kushindwa kuungana na wapigania uhuru wa TANU. Kulitokea kasumba kwa wasomi kuwa  Waafrika hawawezi kujitawala kwani hawakuwa na lolote lile kwani walishindwa kutengengeza kibiriti tutaweza kuongoza nchi kubwa kama hii.

Na hata wale waliokuwa wasomi jiji Dar Es Salaam waliokuwa wanatamani kujiunga na  wapigania uhuru wa TANU. Walijikuta wanakosa nafasi kwani suala la kupigania uhuru lilihitaji muda sana. Na asilimia kubwa ya wasomi walikuwa watumishi kwenye serikali ya mkoloni. Hivyo kulitokea wasomi kuacha kazi na wengine kufukuzwa kabisa. Hivyo walijikuta wakiishi maisha ya shida na yenye taabu nyingi sana.kwa mfano baadhi ya wasomi kama wakina Mwalimu Nyerere kuamua kuacha kazi na kujiunga na harakati za kupigania uhuru. Ukiachilia mbali wasomi pia kuna wanawake waliopata misukosuko kutokana na wanawake hao kuwa na moyo wa kupigania uhuru. Kulikuwa na wanawke kama wakina Bibi Titi. Na ilifikia wakati kulitokea wanawake walioamua kuchukua talaka na kujiunga kwenye harakati za Tanu.

Mbali na wasomi pamoja na wanawake, pia jijini Dar es Salaam, vijana wengi wenye nguvu walionekana kukosa muda na harakati za kudai uhuru. Kwani wengi wao walionekana kupenda starehe nyingi kuliko kazi. Wengi walikuwa wakipanda snaa kucheza miziki ya kimagharibi huku wakiwa na wanawake wa kizungu. Kitu ambacho wapigania uhuru walipata misukosuko mingi katika kuwashawishi vijana hao kujiunga na mapigano ya kudai uhuru.